Kwa ' Upuuzi ' huu usiovumilika kutoka kwa Wasomi wa Vyuo Vikuu kuna haja ya Kujisifu kuwa ni Wasomi?

[FONT=courier new]Sitaki kuvitaja hapa Vyuo husika ila kwa vingi ambavyo nimevipitia hapa Jijini Dar es Salaam nimegundua ya kwamba 95% ya Wanafunzi wake wa Bachelor Degree na Masters Degree researches / dissertations zao wanafanyiwa na Watu ’ Maalum ’ kwa malipo ’ Maalum ’ kisha muda ukifika Wao wanazifuata tu na kwenda kuzifanyia ’ defending ’ katika ’ Panels ’ husika wakimaliza wanakuja ’ Kutamba ’ mitaani kuwa wameelimika na wao ni Wasomi wa Kutukuka.

Tusijidanganye kwa sasa Tanzania hatuna tena ’ Typical Intellectuals ’ bali tuna ’ Fake Intellectuals '. Nimekasirika na kuchukia mno hasa baada ya jana tu nikiwa maeneo ya Sinza kuwaona Vijana fulani wa Vyuo Vikuu vya hapa Jijini Dar es Salaam baadhi wakiwa ’ wanabeti ’ na wengine wakiwa ’ wanagambeka ’ halafu wanawapigia Simu Watu wanaowafanyia na kuwaandikia hizo researches / dissertations zao kama ziko tayari au bado ili wapate Vyeti vyao na wajiite Wasomi.

Acheni tu Wakenya, Waganda na Wanyarwanda watushinde Kielimu na watuache Kimaendeleo hakyanani!

Nawasilisha.[/FONT]

Tatizo la cheating liko kila mahali. Iwe Kenya, au America. Binafsi kuna wakati nilikuwa nawafanyia assignments wamarekani wakinilipa. Huku kenya accounts kwa tovuti kama essaywriters.net( au sijui .com) ilikuwa ikiggharimu hadi KES 60,000. Cha maana ni watu waache kuabudu makaratasi, wajiulize kuhusu skills za mtu

Kweli kabisa kuamini makaratasi kunaua elimu ya ubunifu. Nimilikutana na CPA holder hawezi hata kuandika cheki (cheque). Hajawahi hata kuona Tax Invoice lakini anasema yeye ni mhasibu ana cheti cha NBAA.

Hadi mabango ya kuhamasisha hizo mambo yapo pia hadi vyuoni.Nilishangaa siku moja kuwa kutakuwa seminar (inalipiwa) jinsi ya Kuandika CV.Tena Tangazo limebandikwa kwenye chuo kikubwa tu hapa nchini.Nikajiuliza ina maana huko chuo hakuna sehemu wanafundisha jinsi ya kuandika CV?

Watu wenye vyeti fake lazima wangekuwa smart tu.Mtu ana cheti fake lakini anaijua kazi yake vizuri,mtu ana cheti Og lkn kazi hajui

aiseee umeongea ukweli mno…yaaani na watu wanapigwa hela balaa