Kufunga Mwezi wa Shabani

Kutoka kwa Usama ibn Zaid t Asema: Nilisema: (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijapata kukuona ukifunga mwezi wowote mfano wa unavyofunga Shabani. Akasema: Kwa sababu huo ndio mwezi ambao watu wanaghafilika kati ya Rajabu na Ramadhani, na ndio mwezi ambao matendo hupandishwa juu kwa Mola wa walimwengu, basi napenda matendo yangu yapandishwe hali ya kuwa nimefunga) [Imepokewa na Nasaai.].

Ama Katazo lililo kuja katika hadithi ya Mtume (saw) Inayo sema (Ifikapo nusu mwezi wa shabani Musifunge) [Imepokewa na Ibnu Khuzeymah.]

https://www.al-feqh.com/sw/saumu-funga-za-sunnah