kuanua nguo

Nyumba za kupanga hizi, demu kafua nguo sindiria , chupichupi na kadhalika, kaenda kazini sasa we ndo jirani pekee dume siku hiyo uliepo mara mvua hiyo na nguo zimeshakauka sijui utaanua umtunzie ama vipi na wala hauna mazoea naye.
Tabu sana

Wewe ungefanyaje sasa

ningeacha vilowane hapo hapo heri nusu shari s shari kamili

Tupa kule

Mmh. Unaanzaje kuzianua wakati hukuombwa uzianue?

Wacha zilowane akija atazianika tena. Waweza fanya wema ila mwisho wa siku ukaonekana mbaya.

Unazianua mvua ikiisha unazianika tena.

Aah, mimi naanua tu namtunzia vizuri pa si nashaka yoyote.
Kwani nazo si nguo kama nguo nyingine tu.!!?:cool::cool::cool:

Hahahaaa. Kwani kakuomba sasa rafiki?

Akija kukushushua na kukubwagia mijitusi utafanye au ndio utajutia wema wako?

Na kwanza kwanini ukimbilie kuwaza kuwa atakuja kukushushua badala ya kushukuru?
Ukiziacha akija akilalamika hujamtolea je napo utajilaumuje?
Nguo ni nguo tu Rafiki, zali hilo likinikuta mimi ujue nazitoa.

Hahahaaa. Kwa wale wenye midomo akija akiona nguo zake ziko vululu vululu lazima apayuke tu Mkuu. Hapo ndio utajuta.

Pia nimewaza inatokea una Girlfriend wako mara kaja ghafla na kukuta ukiwa ndio unazianika kwenye kamba hivi utamjibuje hapo Mkuu?

Hahahaaa. Angekuwa na nia ya kuanuliwa angeacha akiba ya maneno rafiki kwamba endapo Mvua itakuja umuanulie. Au nyie hapa mnasemea mvua gani sababu hakunaga mvua ya hivyo kwamba ije tu pasi dalili wala msimu.

Hamna kitu kama hicho rafiki eti alalamike wakati hakukwambia. Mmh.

Nikwambie tu ikikutokea rafiki na hujaambiwa uanue we achana nazo tu. Hahahaaaa.

Rafiki, kuna zile mvua za kushtukiza ndani ya robo saa tayari hapakaliki,
Sio lazima aseme, mbona vitu vingine akiacha mnaweza kumtunzia?
Kwanini nguo uogope.?

Tena nitamtolea kwa Adabu na kuzikunja vizuri kisha ikiwezekana naenda kununua na begi jipya kabisaa nakuja nazihifadhi swafii kabisa.
Akija namwabia bibie mzigo wako huu.!!?
Uone kama hajakuzawadia na kazawadi!!:):cool:

Hahaha temaga mati chini, unajua misaada mingine inaweza ikakuponza na ni ngumu kujitetea na kueleweka.
Aisee bora niziache hapo hapo.

Wacha weeeee. Ila sio kwa wema huo rafiki.

Haya bana kila la kheri. Hahahaaaa. Lol. Nimejikuta nawaza huo muda unaposema bibie mzigo wako huo lol.

Ila una moyo bana rafiki. Inabidi nijage niwe jirani yako aiseeee. Hahahaaa. ( ndukiiii)

Hahahaaa. Umeonaeeee.

Namshangaa @Dam55 anavyolichukulia kiwepesi wepesi sababu mingine huwa ni mitego unaweza fanya wema ila upande wa pili ukajuta kuufanya ule wema.

Doh!! Mbavu zangu masikini dah!!
Karibu sana Rafiki.

Mh! Tatizo lenu nyie mwakimbilia kuwaza matatizo tu, yaani matatizo ndo mmeyaweka mbeli zaidi sijui kwanini.
Hapo unajitoa muhanga tu!!

Hahahaaaa. Lol.

Ila jirani yako mmoja akihama nishutue tu rafiki. Teh teh

Hahahaaa. Vipo vitu rafiki hata iweje asilimia ya kutoleta tatizo ni ndogo mnooo.

Na moja wapo ni hili rafiki. Ingekuwa Mahindi au mchele hapo angalau tungesema sio ustaraabu ila kwa nguo tena za ndani we ziache tu zilowane jua likija zitakauka tena. Hahahaaaa.

Kuna vyumba viko wazi hapa we sema tu lini wahamia.
Mimi nitakukodia gari ya kukuleta.:cool::cool::cool: