Kiranga na Mshana

Fuso

Village Elder
#17
Sikubahatika kushuhudia ubishi huo, lakini kwa kifupi Kiranga anaamini Sayansi kwamba tusiyoyajua leo kuhusu dunia yatapata majibu yake kadri karne zinavyosonga mbele wakati Mshana JR anaamini kwamba haya yote yamefanyika sababu MUNGU hupo na ndiye anayefanya dunia izunguke kila siku bila kusimama wala sec moja, na Jua lisizime wala kuikaribia dunia.....

nimeenda kule nyumbani nikapekua pekua kwa makabrasha nikaona toleo hili, hapa ndipo walipoanzia. Kweli ngoma ilikuwa nzito...


Mshana JR Post yake JF 19th May 2018 kwa hisani ya JF-Home.

Kinara mbishi asiyekubali kuwa kuna Mungu. Mbishi kwa viwango vyote unavyojua ila mwepesi wa hoja.

Kiranga sio atheist, kwa tafsiri rahisi atheist ni mtu asiyejua lolote kuhusu Mungu ama miungu (Hana ABC zozote kuhusu hizo imani za Mungu na miungu)

Kiranga sio mmojawapo. Kiranga ni mmojawapo wa wale waliokengeuka imani, walizaliwa katika ukristo wakabatizwa na kuishi maisha ya ukristo... Lakini along the way wakabahatika kusoma doctrines za kikristo, Mungu nk.

Ni katika hizo doctrines wakashindwa kukubaliana na vifungu kadhaa hivyo wakakengeuka na kuwa wapinga Uwepo wa Mungu mkuu.

Ni watu wenye elimu kubwa kuhusu dini hasa ukristo halafu wakasoma na doctrines nyingine zinazopinga uwepo wa Mungu na kuchagua kuyaamini hayo.

Kipengele muhimu hawa watu wasio waaamini ni kule kutaka wanachokikwepa ni kile cha kutotaka kutambua kuwa ishu za kiroho, Kimungu hazina ithibati za kisayansi.

Wote tuna akili. Je, kuna ithibati? Na kama hatuna akili tuna ithibati? Lakini uhalisia unasemaje?

Kwahiyo Kiranga anataka umuoneshe Mungu as if ni kitu solid. Kiufupi hawa sio atheists bali non believers!!!
 
#18
Kiranga angejibu kuwa "ndio nina akili" basi Mshana angemwambia athibitishe hizo akili.

Huyu jamaa Kiranga Mimi naamini kabisa kwenye uhalisia wa maisha yake anaamini Uwepo wa Mungu ila huwa anachangamsha tu baraza kusema yeye ni atheist.
 

Top