kadoda jizee la 60s from jamiiforum is officially here looking for his kenyan friends in kenyatalk.

nipo hapa kwa ajiri ya kutafuta wale marafiki zangu wakenya niliokuwa narumbana nao kule jamiiforum kupitia jukwaa la kenya.

kama unajiua wewe ni mmoja wapo, weka comment yako hapa.

Wewe mtizedi umekuja bila kugonga hoodi

nipo Atown hapa… na kesho naingia hapo nairobi bila hodi.

Ukuje upambane na wakora wa Nai

karibu kaka…

kama niliweza kuwatoa jasho kule jf, hapa itakuwa kazi rahisi sana.ni kama kusukuma mtu aliyekunywa chang’aa.

Hii Kelele yote na umetishwa na kamzee jiwe, Kenya utaweza kweli?

nimekaribia.

ondoa shaka.

Haya basi, nenda keti na wenzako pale sub-forum ya wakimbizi utegee kopo la uji wa minerals…

nitakuwa hapa 24/7.

@FieldMarshal CouchP umeget company.

:D:D hapa hawawezani… Language barrier…

hii lugha ya kikora siwezi get.

ni kweli, sheng ni lugha ya wakora wa nairobi.

Samahani mkuu.Nakuitia babu mwenzio msemezane.

sawa mkuu, niitie na babu geza ulole.

Huyo hazungumzi sheng aisee, Kisha hio mentality ya eti sheng ni lugha ya wakora ikome. Hio ni lugha ya wakenya…

mbona wakenya wasomi hawazungumzi sheng?.. kwanini inazungumzwa tu maeneo duni ya watu fukara wa nairobi?.

Sasa Hao wasomi ulikutana nao wapi ukazungumza nao, ukagundua kwamba hawatumii lugha ya Kenya aka sheng? Ama ukiwaona kwenye runinga watarajia wazungumze sheng?
Na ndio nikakwambia, punguza mentality ya kikoloni…