Jiungeni Kwa Username Zilezile Kuleta Msisimko

Natoa ushauri was wana Jamiiforums Kule Tanzania kujiunga na mtandao huu kwa majina Yale yale kama BAK, mshana Jr , Elli, matola nk nk ili kuendeleza utamu na muonekano uleule was jf

Taarifa imfikie Geza Ulole popote alipo. Kenya "adui "yako mkubwa will gladly host you and Lumumba lot.

Suala la usalama linatatiza mkuu
Privacy ya humu sio kama ile ya jamiiforums mkuu
Hata mello alitoa tahadhari ya kutumia data zile zile ulizokua unatumia jf ujue unatake risk ila akili kumkichwa mkuu

hehehe,huyo bado anahuzunikaaa

Tuko mkuu tumekuja kwa id zetu zile zile

Mbona Kule jf ulikuwa umejisali kama mchaichai??

Nadhani hili litakuwa limechelewa sasa inatubidi tuitishe locoo huku naanza na mshana> demiss> … …

Kwanza nisaidieni wakuu…tangu jana natafuta namna ya kujiunga nashindwa…kuna hili neno recapture limenisumbua mno…yani hapa nimejiunga kupitia face book

Nakazia

Pamoja mkuu

bila shaka ni uwezo wa simu unayotumia ina uwezo mdg kwaio itabd utafte cm nyingne kwanza ili ujiunge then utaendelea nayo ukishajiunga, ila kama iko poa basi hakikisha unatumia crome au safari unapoanza kujiunga ndo zinakubari recapture, kwa operamin au direct from google utakesha, ila ukishajiunga waweza tumia yoyote

Inapendeza zaidi…

Though usalama ni wa mashaka…

Cc: @Mahondaw

Nimefanikiwa mkuu…
Samsung Grand Neo sii ndogo bana…

Wengine uwoga tu, na ndio tayari tumeshakuja hvo. Mengine yataji sort by default

Nakushauli tumia browser kama google chrome, firefox nk kujisajilia. Operamini sizani kama unaweza vuka hiko kipengele

Aise nimefanikiwa

Kwa kweli itajulikana mbele ya safari lakini kuja ndiyo tumeshakuja. Kinachofurahisha ni mfanano fulani hivi na Jf!

Mfanano ni ule ule maana majukwaa karibia yote yamekamilika.

Na member ingetakiwa tuje kwa ID zetu za JF ingependeza zaidi japo kuna hofu ya usalama na watu wameamua kuja kwa ID mpya(sio vibaya pia)

Kikubwa tuendelee kujadili na kuhabarishana kama ilivyokuwa kule JF, wengi wetu tulikuwa tunaitegemea JF kwa habari mbalimbali kuliko vyombo vya habari kama TV na magazeti.

Hivi hofu ya usalama kinamaanishwa nini? Kwamba watu watakamatwa ama watadukuliwa?

Tuliojiunga hapo kabla itakuwa ngumu kulitekeleza hili, hebu njoja nimwulize @Mundu Mulosi Kama anaweza kubadili ID yangu nitumie ya JF