Jinsi ya kukaanga kitimoto.

Twende moja kwa moja. Tenga kitimoto yako na maji na tia chumvi, wacha ichemke hadi maji yaishe.
maji yakiisha anza kuigeuza geuza ili isigande kwenye sufuria. unaweza weka pilipili kwenye stage hii. endelea kugeuza mafuta yatatoka kwenye mafuta yake(stake tupu haifai).

Geuza hadi iwe ya kahawia, mafuta yake yaliyotuna inabidi uyaminye.

Gonga kitimoto yako.

Duh!..

Vipi mkuu?!

Umenitia njaa, sijapata hii kitu muda mrefu sana…

huku Mbeya hiyo kitu tunakula daily. Kilo buchani 5000 -6000. Karibu sana.

Mimi huwa nachemsha kitimoto na tangawizi kikishaiva…nachukua supu nagonga(nainywa) tena supu ni tamu sana,kisha hiyo nyama naiacha jikoni ikauke halafu naweka mafuta haya ya kawaida naacha ijikaange hadi ikaribie kuwa kahawia kisha naweka vitunguu maji na thaumu halafu naongeza nyanya za kawaida baadae kidogo naweka tomato paste naendelea kukoroga hadi inatengeneza rojo halafu naweka mbogamboga naendelea kukoroga nikishaona mboga zaimeiva naweka ndizi zilizorostiwa au chips au magimbi mekundu yaliyochemshwa…nikishaona ile rojo imeshaanza kukolea kny hizo ndizi au chips naipua tayari kwa kula…hii kitu inaendana na bia,k-vant,konyagi hata mbege siyo mbaya.

picha muhimu Wadau haswa sisi Majirani ambayo kiswahili kinatupiga chenga.

[ATTACH=full]180484[/ATTACH][ATTACH=full]180485[/ATTACH][ATTACH=full]180486[/ATTACH]

Hapo mwisho hapo mwisho…!

[ATTACH=full]180499[/ATTACH]

Ewaaaaaa…

Hii style ya kupika iko vipi?

Roast in oven

Nimeipenda

Mkuu next time uwafundishe watu kutengeneza kisusio cha Nguruwe pia…

Hiyo kitu kuna jamaa yangu ni mtaalamu wa kukiandaa ngoja nikipata nafasi nitambelea anielekeze namna ya kukiandaa manake kisusio cha kitimoto nikitamu kuliko kitimoto chenyewe.

uko vizuri, tatizo kwenye supu tu Siwezi kuinywa

Aiseee umeniharibia siku, siwezi kula chochote leo hadi niitafute hii na hela sina

Nyama ya poku yenye mifupa mingi nitamu kinoma…jaribu utaniambia.

tatizo mafuta mengi