Je naweza kujua kama siyo kufahamishwa Mafunzo ya Walinzi wa Marais duniani huwa yanakuwaje?

[FONT=courier new]Mwanangu GENTAMYCINE jr kila anapokuwa akiwaona Walinzi wa Marais kama vile Trump, Kagame na Magufuli vile wanavyokuwa wanawajibika katika matukio yao kadha wa kadha huwa anafurahi sana na ananiuliza Baba yake Mimi ni wapi huwa wanafundishwa ili nimpeleke ila swali ambalo kiukweli kila mara amekuwa akinisumbua kuniuliza na sasa linanichosha hasa ukizingatia Mimi sijui lolote na huwa sipotezi sana muda kuwafuatilia hao Watu ni kwamba mpangilio mzima wa ’ Mafunzo ’ yao hayo huwa ni yapi?

Kama kuna mwana JamiiForums aliye ndani ya Kenya Talk anayejua basi anisaidie kunijibia hili ili nami GENTAMYCINE jr akirudi kutoka zake ’ Tuition ’ baadae niweze Kukizi ’ Kiu ’ yake ili basi wakati akiwa bado anakua aweze kujua ili nae aje kuwa ’ Mlinzi ’ wa Rais huko mbeleni anatakiwa aweje na kubwa ajiandae na aina gani ya mazoezi na mambo mengine yenye umuhimu.

Tatizo kubwa ni kwamba Baba yake Mimi sijasoma na Elimu yangu ni ya ’ manati ’ mno na ninachojua tu ni Kazi zangu za Ukulima, Uvuvi na Ufugaji zinazonipa Kipato hivyo huko ambako anataka kunipeleka Mwanangu GENTAMYCINE jr wala sikuwezi na naogopa anaweza pia kujua Mimi ’ Babaake ’ ni ’ Ngumbaru / Mjinga ’ wa Kutukuka kama nisipompa majibu ya kutosha juu ya maswali yake hayo Kwangu.

Nisaidieni jamani nisiumbuke mbele ya Mwanangu huyu!

Nawasilisha.[/FONT]

Mkuu Senior Villager GENTAMYCINE, hakika hii ni elimu nzuri sana, ni swali linalofikirisha…

Kitu ambacho sijaelewa ni kuwa huyo Gentamycine Jr anauliza kuhusu nani hasa, yaani huyo anayemaanisha ‘mlinzi wa Rais’.

Kama anamaanisha yule Ofisa wa jeshi mwenye sare ambaye siku zote huwa anasimama nyuma ya Rais, basi nijuavyo yule siyo mlinzi bali ni ADC, ambaye shughuli yake ni kuwa karibu na Rais kwa mambo mbalimbali ya kijamii na kazi kwa Rais, kama kubeba hotuba kwa Rais, kuangalia kiti kimekaaje na ni symbolic gesture ya madaraka ya Rais. Ila si marais wote wana Ma-ADC, mfano Rais wa Marekani. ADC huteuliwa na Jeshi ingawa pengine Rais akawa na ‘ushawishi’ katika uteuzi wake.

Lakini kama anamaanisha wale walinzi wa kiukweli ambao hawavai sare, ni kwamba wanakuwa na mjukumu tofauti ingawa yupo mmoja au wawili ambao huwa karibu na Rais, na walinzi hao/huyo walio karibu na Rais hawachaguliwi na Rais.

Kikosi cha ulinzi cha Rais ndicho kinamteua mlinzi huyo kutokana na vigezo mbalimbali ikiwemo ukakamavu, ujuzi wa mafunzo ya mapambano (martial art) kama karate, utiifu wake kwa system na kwa Rais, muonekane wake n.k.

Nadhani wajuzi wa haya mambo watakuja kujazilizia au kudadavua…

Kwani kwa nini wanalindwa

Hilo swali sidhani kama mtu anaweza kulijibu hata akiwa mmoja wao, nadhani kikubwa ni kujua utaratibu wa kujiunga na mafunzo hayo.

[FONT=courier new]Kwanini unawasemea Watu Mkuu? Wamekuambia kwamba hawawezi kujibu? Ni mara ngapi Watu wamekuwa wakiuliza mambo tena yaliyo ’ Nyeti ’ kabisa humu humu JamiiForums ( japo sasa tumehifadhiwa kwa muda na Uhuru Kenyatta na Kenya Talk yake ) na bado tumekuwa tukipata majibu yaliyo Kuntu / Sawia kabisa?[/FONT]

Sijawasemea mkuu, comment yangu sio conclusive, hebu itafakari vizuri

[FONT=courier new]But it looks so ’ conclusive ’ Chief! Have they ’ employed ’ you as their Spokesman or Spokeswoman?[/FONT]

Really?! Then I rest my case! I don’t want to add a number of posts that aren’t related to the content.

hahahah anakuchokonoa? samahani kwa kutumia kiswahili ambacho kinaweza kutafsrika vibaya.

pamoja na mafunzo wanayopata nje ya nchi wana jengo lao pembeni kidogo ya mji ambako upepo mwanana huvuma na huko ndiko wanako kazia(baada ya kupata yake basic ndani na nje ya nchi) mafunzo yao

Mbuzi beach…!!! Karibu na kijiji ambacho wakiweka kituo cha Polisi hakichukui muda wanakiondoa…!!! kwa wakati huo wa miaka ya 1989…!!!

Niliambiwa kuwa huyo mlinzi pia ni lazima awe marksman mwenye shabaha hakosi target.

Mlinzi yupi? ADC au wale walinzi wengine? Maana wamegawanyika kulingana na majukumu waliyopewa. Ila suala la shabaha ni moja ya vigezo muhimu…