Itakugharimu ukifanya au usipofanya

Habarini wana bodi.
Kuna vitu ambavyo huwa vina ‘outcome’ positive na negative iwe umefanya au hujafanya. One of it ni neno moja tu,’ Maamuzi’
Kuna baadhi ya mambo ambayo kama mtu hutayafayia juhudi kukabiliana nayo ni ngumu sana kuishi positive, ni mgumu pia kushape na kudirect maisha yako vile unapenda /ungependa yawe. Maamuzi ni kitu muhimu. Wengi wameandika na mengi yamesemwa ila nami ningependa kutia neno.
Niliwahi soma A ‘Start-up Nation: The Story of Israel’s Economic Miracle, 2009 by Dan Senor and Saul Singer about the economy of Israel.’, ni moja ya kitabu ambacho waandishi wanaelezea kwamba ‘Maamuzi bora’ ndio chachu ya uchumi imara wa taifa la Israel ni, ‘Maamuzi’ walio kuwa wakifanya viongozi wao katika nyakati zote na hasa nyakati za vita.
Moja ya falsafa ya IDF (Israel Defense Force) ni kwamba, kwenye battle field na hata kwenye maisha, Kila mwajeshi yuko ‘responsible kwa kila kinachotokea na kila ambacho hakitokei kwenye maisha yake /eneo lake la kazi’. Maamuzi haya ya kuwajibika in either direction yamewafanya wapige hatua kubwa. No blaming others, no excuses.
Wakati flani kuna muandishi wa habari aliwahi mfanyia interview CEO wa kampuni moja, na moja ya swali lake kwa CEO huyo lilikua, ‘ni nini siri ya mafanikio yako’?, CEO alijibu simple tu, kwamba, ‘Good Decision/Maamuzi sahihi’. Yule jamaa akamuuliza tena, unafanyaje maamuzi sahihi, CEO alijibu, ‘through experience’…kwa hamaki muandishi akamuuliza, ‘how do u get that experience??’, CEO akatabasam then akajibu, through ‘Bad Decision’!
Kwenye maisha haijalishi ni kipi au lipi unafanya, maamuzi yako be it kwamba ni mabaya au mazuri will take u somewhere ‘unapotaka kufika na usipotaka kufika’. Kitakacho kutofautisha na wengine in a positive way ni kwa kiasi gani 'experience yako ya maamuzi au kwenye eneo flani la maisha yako imekufanya kuwa a ‘responsible human being.’ Kuna Mengi tunayafanyia maamuzi daily lakini hayajabadilika na tunaishia kuwalaumu wengine wakati shida ni sisi wenyewe.
Maamuzi mazuri, Experience na kuwajibika kwa kila kinachotoea na kila ambacho hakitokei kwenye maisha yako that’s the key. Blaming someone won’t pay your bills.

  1. Kuna wale rafiki zangu ambao you’ve lost everything. Ngoja nimwambie kitu, losing everything that means huna kingine cha kupoteza, learn to Risk Big coz you’ve nothing to loose. It ain’t easy though ila pia hayo ni maamuzi yako. How u’ll do it is non of my business ila as long as bado uko hai that’s a ‘proof’ kwamba you still have a chance to do something. Something positive. Go and risk Big.
  2. Kwa wale ndugu zangu mliopata kazi na mliopo makazini, jifunzeni kujua nini mnahitaji kutoka katika hiyo kazi then Leave that job. Don’t kill yourself for a job ambayo inaweza kukureplace within a week or two when you drop dead. Leave and take care of yourself, establish something of your own. Haitakua rahisi pia, ila ni maamuzi yako kufanya. And be responsible for it.
  3. Kwa wale ndugu zangu ambao hamjui kipi mfanye na kipi msifanye, punguzeni 'options za mnayotaka kufanya na yale msiyotaka kufanya pia. Ile kwamba unaweza fanya jingine endapo moja litafail inakupunguzia ufanisi na umakini wa 'kufanya moja mwanzo mwisho ’ utakua unajiaminisha kwamba unayo ‘safe haven’ ya option B. Sio mbaya kuwa na place to go when things are not doing well, ila ni vema pia kujipima kwa kufanya jambo moja hadi ukalitimiza. Kabla Marck Zuckerberg hajazinunua WhatsApp na Instagram alihakikisha kwamba ‘The Facebook’ inaitwa ‘Facebook’, chimba eneo lako, hakikisha hakuna jiwe ambalo halijapinduliwa then nenda eneo jingine. Hayo ni maamuzi yako kufanya pia na unawajibika kwayo.
  4. Kwa wale ambao mmefanikiwa katika yale mnayo fanya, niwakumbushe tu kwamba, huu ndio muda sahihi wa kuanza kitu kingine kipya. An average millionaire anazo source zaidi ya saba zinazo muingizia kipato. Adui moja wapo mkubwa wa next level of success ni current level of success. Mafanikio hupumbaza na kumfanya mtu ajihisi amefika. Don’t limit yourself, you still have a chance kufanya mengine mengi. Invest in yourself, go places, read a book you haven’t read. The onus is yours na ni maamuzi yako kufanya.
  5. Kwa wale ndugu zangu mliograduate na mtakao graduate soon, it’s time sasa kutumia mlichojifunza though most of what you learned (kwa mtazamo wangu) it was meant for industrial era, saivi things have changed. Nilishangaa kumuona Prof akimaind kwamba Bitcoin Investment is not something worth kisa price inaincrease kwa muda mfupi lakini Prof huyo huyo anaita ‘Class education’ good investment while the price of collage tuition imekua ikichange since alipokua bado chali mdogo na hajastuka. The major issue ikiwa ‘Time’.
  6. Kwa wale ndugu zangu msiojiweza vitandani, well, that’s the time ya kureflect back uliokuwa unafanya. It’s also an opportunity to think and plan what next. It time kuyatengeneza na Mungu wako pia (for God’s believers), kwamba akikuita unakua safe, na akikupa chance ya kuishi tena basi unanza kufanyia kazi uliokua unaplan while in bed. Every minute is precious.
  7. Na hatimaye kwa ndugu zangu mnaomiliki gadgets mbali mbali, you guys are lucky. You’ve got something to start with, be it simu, laptop or anything that can connect you with the world. Anza na ulichonacho, make it useful.
    Ni maamuzi yako kufanya au kutofanya chochote. Nothing blooms all year round, everything has its own timezone, and this might be your year of blooming, ila ni maamuzi yako kuufanya mwaka huu uwe positive au ubaki history kama miaka mingine yote iliyopita.
    Maamuzi sahihi na kuwa responsible kwa kila kinachotokea na kile ambacho hakitokei kwenye maisha yako that’s the only key…
    Siku njema!!!
    Credit#Sci-Fi

Ndefu sana na nzuri sana, kuisoma hii yote ni maamuzi sahihi na magumu

Okay!..

Safi Sana kwa kutukumbusha…! Jf halisi inaanza kuonekana sasa

Ujumbe mwanana.

ndio maana niliimisi jamii forums. nanukuu kwa kutilia mkazo kilicho andikwa hapo juu

“…CEO huyo lilikua, ‘ni nini siri ya mafanikio yako’?, CEO alijibu simple tu, kwamba, ‘Good Decision/Maamuzi sahihi’. Yule jamaa akamuuliza tena, unafanyaje maamuzi sahihi, CEO alijibu, ‘through experience’…kwa hamaki muandishi akamuuliza, ‘how do u get that experience??’, CEO akatabasam then akajibu, through ‘Bad Decision’!..”

nakazia zaidi…

“…Kwa wale ndugu zangu mliopata kazi na mliopo makazini, jifunzeni kujua nini mnahitaji kutoka katika hiyo kazi then Leave that job. Don’t kill yourself for a job ambayo inaweza kukureplace within a week or two when you drop dead. Leave and take care of yourself, establish something of your own. Haitakua rahisi pia, ila ni maamuzi yako kufanya. And be responsible for it…”

Haya madini adimu saaana.

thanks sana… naanza wikiend vzr…

Wastaafu wengi hufeli kwenye kuwekeza pesa zao kwasababu ya kukosa experience. Ni vizuri mara tu upatapo ajira uanze kuwekeza kwenye miradi mbalimbali. Hii itakupa experience na utashangaa jinsi unakuwa tajiri. Ukipata kazi usikimbilie kujenga au kunua usafiri wa kutembelea. Utakopa utajenga, utakopa tena utanunua gari…kufumba na kufumbua miaka 50 hii hapa.

Hapa nimeparudia zaidi ya mara mbili

Ndefu wanasema ndio nzuri Mkuu.

Hapana aiseee inaumiza

Kusoma au:p:p

Ndio mkuu au niseme macho yanaumia

Ukiona unafanya kazi then unaendelea kukonda na afya kudhoofu hiyo kazi haikufai iache iakuua…!!!