Ilishawahi kukufika hali kama hii

Rafiki yako wa karibu ambae amekusaidia laki tano, uliahidi kuzirudisha ndani ya miezi mitatu. Sasa ni mwezi wa sita hujarudisha. Si kwamba hutaki ila hesabu zimekaa vibaya sana.

Unahitaji laki saba sasa hivi, pamoja na laki saba, huyu rafiki amekusaidia freezer yake ambayo haitumii ili anagalau uuze barafu ikutoe katika mawazo ya pesa ya mboga kila siku.

Umerudi tu na laki saba, mtoto ametengua mguu, umemkimbiza hospitali inabidi apigwe X-Ray kuangalia kama mguu umevunjika. Baada ya matibabu laki tatu imekatika ambayo hukuipangia budget.

Ile shida ya mwanzo iliyokufanya uombe laki saba iko pale pale. Unajua rafiki yako anaweza kukusaidia lakini sasa nafsi yako inakusuta.

Ombeni Mungu kwa kila jambo…

Bima ya afya ni muhimu

hiyo inaitwaa siku ya kufa nyani…

Haya huwa yanatokea kilichopo ni kupambana na hali

Marafiki kama hao ukiwa nao ni wakutunzwa

Ukiona hali kama hiyo inakutokea, kaa chini utafakari ni wapi umekosea. Hakuna kitu kinachokuja tu hivihivi pasipo sababu au kusudi la Mungu…

hakuna wa kumrudia zaidi ya mwenyezi Mungu mwingi wa rehma

unaweza mfukuza mkeo ukizani ndio anayekutia mikosi, mtihani huo ni mdogo sana kwa tunayopitia…nakumbuka kuna siku nilipata laki sita nikalipa kodi kisha jioni ya siku hiyo nilinunua simu mkonoi nikiwa na nia ya kuja kuiuza kwa bei ya juu zaidi, niliiuza laki nne huku mimi nikiwa nimenunua laki tatu, asubuhi siku inayofuata anakuja yule mdada aliyeniuzia na polisi, nakamatwa kwa kosa la wizi wa simu na mengine kibao, huko polisi nikalala, nikalala tena na tena, nakuja kutoka ikanitoka kama mia saba hivi na simu ile ikachukuliwa, narudi home naambiwa mke wangu yupo hospital kajifungua salama ila mtoto mmoja bahati mbaya, sijakaa vizuri yule nilimuuzia simu ananipigia anahitaji arudishiwe laki nne yake, pale hiyo siku sitoisahau…

Aisee hii ni noma sana

Maisha ni mtihani

Kuna muda nilipitia mtihani lakini Mungu ni mwema sikuadhirika Ila nilichopata kilitosha mahitaji muhimu tu.
Mama aliniuliza bipod hali yako, nikamjibu mama kikubwa nina furaha na amani.

Pole sana mkuu.

tremendous shukran mkuu

Hii mitihani usiombe ikutokee

Sidhani kutokewa na hali kama hizo ni lazima kuwe na mahali umekosea. Ni hali za kawaida tu katika maisha. Tena wakati mwingine unakuta hali kama hizo zinakutokea bila ww kuwa chanzo cha hali hiyo.

Huyu mleta uzi kaongelea tu hali hiyo ya ugumu lakini hajaongelea hali ya mambo kukunyookea. Kuna wakati mambo yanakunyookea kwa kika ufanyacho. Unakuta upepo umekunyookea hata ukifanya jambo la kawaida kabisa unafanikiwa. Kwa uzoefu wangu mimi ninapokutana na hali ngumu huwa wangalau ni kama miezi 6 kisha nakutana na mambo mazuri, na hali hizi zote mbili nazitambua na jinsi ya kuziishi.

Maisha inakuwa kama safari ndefu, huko barabarani unakutana na milima, miteremko, tambarare nk na bado safari unafika. So mleta mada kaelezea tu upande wa mlima na sio mteremko.

Nina experience na mambo haya. Na hata mambo yanapokunyookea ni lazima kuna sababu (ambayo si lazima uijue, ndiyo maana wengi ambao huwa hawafanyi utafiti baadaye hurudi kulekule kwenye msoto). Hakuna jambo linalotokea pasipo sababu (kama utazama kwenye tafakari ya kina katika kutafuta ukweli wa maneno yangu utanielewa…

Dada I guess hii hali imewahi kukutokea so umeleta kisa cha ukweli au karibia na ukweli. Hayo ni mapito tu. Ukikutana hali kama hiyo hapo ndio utajua kama una watu ama la. Katika hali kana hizi ndio unaweza kupima uimara wa mtu kukabiliana hali ngumu.

Katika hali kama hizi unapaswa kutuliza saikolojia yako ili uweze kuvuka salama, kwani kama utashindwa kuchanganua kipindi kama hiki hapo ndio utafanya mambo ya ajabu na watu kuanza kukucheka kwamba umefulia. Usipokuwa makini maisha yako yanaweza kuvurugika kabisa, na iwapo ulikuwa mtu wa kujikweza utahisi dunia imekuangikia na unaweza kuishia kwenye ushirikina.

Sipingi hata kidogo unachosema. Nilichojaribu kusema sio lazima uwe na mahali ulipokosea kwa mantiki ya kwamba wakati mwingine ni sababu ambazo ziko nje ya uzembe au uwezo wako. Baadhi ya sababu za kukuangusha huweza kuwa ni majanga ya kibinadamu, kupoteza ajira, mabadiliko ya sheria hasa za nchi zinazopelekea shughuli yako kukwama, mabadiliko ya tabia za jamii inayokuzunguka nk.

Hiyo hapo juu ni mifano michache tu. Si wote wanaoanguka kwenye maisha wanasababu zilizosababishwa na kukosea kwao. Pamoja na huu utetezi wangu haimaanishi sababu ya kukosea haipo kwenye kuanguka kwako.

Kila kinachokupateni ni kichumo cha mikono yenu. This is a fact