Ikitokea baba mkwe amekutongoza utamwambia mume wako?

Maana kuna wanaume adabu na haya walizisahau kwenye matumbo ya mama zao. Baba mkwe anataka aonje utamu utafanya nini?

Nakaa kimya…ila nitajaribu kukaa mbali na baba mkwe…namkwepa

Maana ukimwambia mumeo atajua umeshaliwa

binafsi…kitendo cha partner wangu kuniambia mtu fulani amenitongoza huwa sikisapoti kwasababu kama angemkubalia huyo mtu sidhani kama hizo taarifa za kutongozwa ungezisikia.

wanawake wamejaaliwa vifua vya kutunza mambo mengi sana, ili kuepusha chuki na migogoro kwenye familia ni kheri kukaa kimya ili maisha yaendelee kama mlivyokuwa mkiishi awali

Humwambii, utakua umefanya ustaarabu mkubwa sana, hata kaka au mdogo wake akikutongoza usimwambie. Ila rafiki wa karibu wa mume akikutongoza mwambie, ili ajue jamaa ni snitch kiasi gani

Ukiona mwanamke anapenda kukwambia flani kanitongoza ujue huyo ana mambo mawili au zaidi.

Moja anataka kukuaminisha kuwa yeye ni mwaminifu sana ili usimtilie shaka hata siku ukiskia tetesi, maana atasema “Mbona huwa nakwambia mtu akinitongoza iweje huyu nisikwambie”

Pili ana mpango wa kukukosanisha wewe na huyo mtu,

Busara ni kukaa kimya na kupambana hali yake dhidi ya huyo anayemtongoza.

Huo mtihani unaohitaji zaidi hekima kuliko mihemuko…

ba mkwe wa namna hii kuna mawili, ana mfadhaiko ama ni jobless, au mzee baba uwe unaishi kwa wazazi.

Unaanzaje kwanza?! Sio baba mkwe tuu hata mwanaume yeyote akikutongoza huwezi sema!

Huwa naona akiona mtu anamtongoza anakupa simu mpokee huyu ananisumbua. Hapo si ushasoma barua ndani ya bahasha? Maisha mvurugano tu

naona kila mtu na hoja yake .hahahaha.

Nikitongozwa siwezi kumwambia mtu yeyote yule kwanza niseme ili iweje.

Sasa kumbe mpaka namba washapeana!

unakula buyu tu but unakaa mbali nae. mita 10000000000

cc @Smart911

Kufa nalo tu usiseme

Nunga hoja mkono

Kwa mfano akimwambia mumeo kuwa unamtaka ? Na mumeo akaamini utafanyaje hapo?
Hii niliiona kwenye movie.

mie akinisumbua sana namwambia

Mimi siwezi kumwambia ,usijekua chanzo cha migogoro ya familia buree. Ni kukaa mbali naye tu huyo baba mkwe.

Sio vyema kumsemea, mumeo hatokuamini

Naona yamekukuta…angalia baba mkwe asije kala °