HUYU MCHUNGAJI YUPO SAHII AU HAYUPO SAHIHI

[SIZE=7]Paul Ogalo: Kasisi wa kanisa Katoliki aliyevuma kwa rap asimamishwa kazi Kenya[/SIZE]
Kasisi mmoja wa kanisa Katoliki nchini Kenya aliyepata umaarufu kutokana na mtindo wake wa kutumbuiza kwa kutumia muziki wa kufoka amesimamishwa kazi.

Paul Ogalo aka ‘Sweet Paul’ amekuwa akitumia muziki wa rap kama njia ya kuwavutia vijana wengi kufika kanisani.

Alikuwa amesema muziki ni njia mwafaka sio tu kuwavutia vijana bali pia kueneza Injili.

Mistari ya nyimbo zake huwa kwa mfano: "Kujeni church kuna baraka, kujeni church kuna baraka…" au "Father Paul, niki-lock kwenye mic, Nduru inafuata, mamanze go tipsy, vijana ruka ruka swag ya kunguru, au sio"
Lakini hatua yake hiyo inaonekana kutowafurahisha viongozi wa kanisa Katoliki magharibi mwa Kenya ambao wamemsimamisha kazi kwa mwaka mmoja ili “ajitafakari”.

Askofu wa jimbo la kanisa Katoliki la Homa Bay Philip Anyolo amesema padri huyo ni lazima achague kati ya kuwa „rapa na kuwa padri".

Amesema kasisi huyo hataruhusiwa kuongoza ibada ya misa kwa kipindi cha mwaka mmoja ingawa anaruhusiwa kushiriki ibada, na pia anaruhusiwa kufanya ibada ya misa lakini faraghani.
[ATTACH=full]179518[/ATTACH]

Aisee

Hii dunia ina mambo…

Ndugu zetu vituko Hata haviishi

taratibu tupo kwao kwao hapa:D:D:D:D:D:D

Kenya kwa vituko mko vizuri.!

kama sio dhambi ni poa tu!

Mbona hana sura ya kichungaji

Mi nadhani wamemuonea. Hip hop sio dhambi kama mashairi anayoimba hayana maneno mabaya

Nadhani hizi Ni mbinu zinamsaidia kueleweka zaidi.
Walomsimamisha wajitafakari zaidi…waingie kanisani waulize kama wanamwelewa au laa

Wakenya hawako Na sura muzuri…

Ujue sisi ni wakimbizi kwao. Tutafurushwa sasa hivi na sijui kama kuna UNHCR ya mtandaoni.

Yupo sahihi kabisa. Hata Yesu alisema alikuja kwaajili ya wenye dhambi na sio waliookoka