HIVI MABINTI WENYE AKILI ZA HIVI, KICHWANI KUPO TIMAMU?

Kwanza kabisa niwasalimu wanajukwaa, habari za muda huu. Natumai mu wazima, mimi pia nina siha njema. Shukrani kwake Jalali kwa kutujalia pumzi njema.

Kitu kilichonisukuma, kikanihimiza, kikanihamasisha hadi nikaweza kufungua uzi huu ni hii tabia ambayo nimeishuhudia kwa baadhi ya mabinti haswaa niliyokutana nao njiani kwenye safari za hapa na pale. Kwakweli nashindwa kuwaelewa, kiasi cha kufikia kuwatafsiri ni wenye matatizo kwenye sehemu kadhaa za bongo zao.

Mmojawapo nilikutana naye nikitoka jijini Dar kuelekea Moro, ndani ya basi la BM. Huyu alinikuta tayari nishaketi kitini, simu ipo mkononi naperuzi.
Ukaaji wake wa nguvu kitini, ukanifanya nimtazame. Tukagongana macho, nikampa salamu maana si vyema kuketi pamoja safarini pasipo walau kusalimiana. Mrembo akanijibu kwa uchangamfu, kisha ‘nikala boksi’ maana huwa si mwongeaji sana haswa kwa mtu nisiye na mazoea naye. Basi safari ikaanza, kufika kibamba tu. Kafungua mkoba wake katoa korosho za kuchomwa na juisi ya chupa. Kanikaribisha, bila hiyana nikashukuru ila si kukaribia. ‘Nikamlia bati tena’ nikawa naperuzi mtandaoni. Haijafika mbali kaanza uchangamfu na kuongea, nikaamua nimuunge mkono asijihisi vibaya. Ndipo nikajua mdada huyu ni mota ya kuongea, nikawa naenda naye sawa. Haujapita muda kaomba simu yangu, kaandika namba zake akasave na kujibip. Nikabaki nashangaa tu, akahamia kwenye SMS napo ni hivyohivyo.

Mwishowe akalala, nikashukuru nami nikajiegesha maana nilishachoka anahama mada hii na nyingine kama mwimbaji anayebadili ‘Melody’ kuendana na ‘beat’.

Basi alipoamka si akadaka simu yake, kuendelea ‘kuchat’. Nikafanya kosa la kutumia uchangamfu, yaani anajieleza mno hata mengine hakuulizwa.

Basi Alhamdulillah tukafika Msamvu, bibie akachomoka garini kama vile gari la wagonjwa linawahi mahututi kwenye ajali. Mimi nikawa sijali sana nikashuka, kisha nikamtumia ujumbe ‘kwaheri’. Maana hakuaga ikabidi niage tu, nguvu kubwa aliyoitumia garini kunizoea isingekuwa viziri

Afanalek! Naulizwa kwani ninataka nini, mara kujuana kwenye gari isiwe nongwa. Mara kila mtu si kamaliza safari yake, sasa wewe vipi.

Yaani SMS zikaongozana kama msafara wa JPM, nikajikuta nikicheka tu maana niliona nachat na mgonjwa wa akili.

JAMANI WANAJUKWAA AYA MBILI HIZO ZA MWISHO NDIYO DHUMUNI LA UZI HUU, NIWIENI RADHI KWA KUWACHOSHA NA MAELEZO MENGI. HIVI HUYU AKILI ZAKE ZIPO SAWA?

SI HUYU TU YUPO MWINGINE NILIKUTANA NAYE KWENYE MKUTANO WA JPM SUA, NAYE KATOA NAMBA HAKUOMBWA NA MBWEMBWE KIBAO. CHA AJABU ANAAGWA TU, ANALETA UJINGA.
WAPO NA WENGINE KADHAA NIMEAMUA NISIELEZE ILI NISIWACHOSHE.

teeeh hawako sawa hao …mwanamke anaejielewa hawezi fanya hvyo
kuomba tu no atasubiria umwombe

Huenda ni nusu timamu

Ulikosea kumwachia akashika simu yako na kusave number yake…
Next time uwe mkali usiwape mwanya wa kukuzoea hivyo.

Wanawake wengi kipindi hiki wapo race sana vichwani…sijui tatizo ni nini

Mimi kuna mmoja nilimtongoza akagoma,nikamlia buyu,sasa hivi ananiangaliaga vibaya as if mimi ndo niliyeleta njaa kwenye hii dunia

Huyo alikupima msimamo si kwamba alikataa

Sasa kiongozi ulitaka niwe mbogo kwenye basi, si kumdhalilisha mtu huko

true

Usipende mazoea na hao viumbe unless uwe unataka papuchi na ume plan, otherwise don’t give a f**k

Wala usingekuwa mbogo, ungemnong’oneza tu angeelewa…
Mpaka mtu anachukua simu mkononi kwao ina maana ulijiachia sana wewe…

Nahisi mawigi na madawa dawa wanayopaka kichwani nayo yanachaingia kukausha akili

Tatizo nimezidi kuwa peace kupitiliza, nahisi hilo ndo tatizo

Hata mimi naanza kuingiwa na shaka juu ya hilo

Basi usiweke lawama kwa Mdada, kumbe wewe ndio mwenye kosa.
Next time ongeza u serious kidogo, hawatakusumbua…

Pole sana…

Wanawake ndiyo walivyo…

Cc: @Mahondaw

Alitaka ugonge korosho akuibie.

Haha… majaribu ni mtaji smart wangu

Kama mtu umempenda utasubiri akuombe namba? Unajiongeza mwenza. Sema huyo wa basi la BM mtambo

Hahah!! Alikua hataki kuonekana maharage ya Mbeya

hahaa utamwombaje mweza ebu nifundishe ndo umekutana na kauzu yuko busy na mambo yake