Tumemsikia Kamanda wa kanda maalum ya Dar, Lazaro Mambo sasa, akitueleza kuwa wale waliiokuwa wakituhumiwa na mauaji ya mwanafunzi, Akwilina, aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala, wameachiwa huru
Lakini Mimi sitajikita zaidi kwenye huo uamuzi aliofanya Kamanda Mambosasa, bali nitajikita zaidi kuangalia kama uamuzi wa kupiga risasi za moto moja kwa moja ulikuwa sahihi
Ninavyojua Mimi kabla ya operesheni yoyote ya kuzima maandamano, kuna taratibu ni lazima zifuatwe
Taratibu zenyewe ni hizi zifuatazo:-
Kwanza kabisa Mkuu wa kikosi kile cha kuzima maandamano hayo ni lazima awatangazie waandamanaji hao (huku akiwa anapeperusha bendera nyekundu) kuwa hayo ni maandamano haramu, kwa maana hiyo wayavunje
Analazimika Mkuu huyo wa kikosi, kurudia tangazo lake hilo zaidi ya Mara 3
Akiona bado waandamanaji hawataki kuitii amri yake, atayaagiza magari ya washawasha ambayo amekuja nayo kwanza kumwaga maji ya washawasha.
Akiona bado waandamanaji hao hawataki kutii amri yake, atalazimika kuamrisha hao askari kupiga risasi za Plastic
Hatua ya mwisho kabisa na baada ya kuona waandamanaji wanajibu mapigo kwa kikosi hicho na hivyo kuhatarisha amani, ndipo anapoweza kuamrisha hao askari wapige risasi za moto, tena siyo kwa nia ya kuuwa, Bali kupiga miguuni kwa lengo la kidhoofisha waandamanaji hao
Swali langu la msingi hapa ni je hatua zote hizo zilichukuliwa, kabla Mkuu huyo wa kikosi hicho cha kuzima maandamano yale kuamrisha aakari wake wapige risasi za moto??
Naungana na BAVICHA kutoa wito kwa Rais Magufuli aunde Tume ya kijaji ili iweze kuchunguza tukio hilo la kusikitisha sana lililosababisha kifo cha Mpendwa wetu, mwanafunzi wa NIT, Akwilina Akwiline