Nchi ya Tanzania kila amayemsema vibaya Magufuli anapata kibano
Walianza na Bunge lililokuwa linaonyeshwa Live, alipoingia tu madarakani akalipiga “ban” ili lisionekane
Akaja kwenye vyama vyote vya upinzani akiwapiga “ban” kuwa wasifanye mikutano yoyote ya siasa hadi mwaka 2020!
Wakati anafanya hivyo kwa wapinzani, hususani kwa chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, yeye kila kukicha anatembea nchi nzima akiitangaza CCM kwa kivuli cha kufanya ziara za kiserikali!
Baada ya hapo akayapiga “ban” magazeti ya uchunguzi ya Mwanahalisi na Mawio!
Huyu Magufuli anachofanya ndiyo kile kitu alichowahi kutuambia Mwalimu Nyerere kuwa mtu aliyeonja nyama ya mtu hataacha kuila nyama hiyo, hivyo anaendeleza ubabe wake na safari hii kaamua kufungia mitandao ya kijamii, inayoendeshwa nchini Tanzania
Lakini alichosahau ni kuwa teknolojia imeifanya Dunia iwe kijiji, sasa katupiga “ban” Tanzania tumeibukia nchi jirani ya Kenya, tukiwa na ari mpya, kasi mpya, ya kumng’oa huyu dikteta Magufuli ambaye seraTamzani kukataa kata kata kukosolewa kwa aina yoyote ile!
pia mavi ya paka ukichanganya na tarasimu fulani ukasimama katikati ya njia panda usiku wa manane utakuwa na uwezo wa kuona wachawi na kila kiumbe kinachotembea usiku.
Halafu huyu Magufuli anaposema No research no right to speak, Mimi simuelewi kabisa, kwa kuwa yeye ndiye ambaye huwa anatuingiza “chaka” kuhusu data ambazo huwa anatupaga
Mfano aliwahi kutuambia kuwa alipoingia madarakani mwaka 2015 alikuta sukari shilingi 5,000 hivi kweli anatudanganya mchana kweupe kabisa, hivi kama kuna mtu anao ushahidi wa sukari kuwa bei hiyo mwaka 2015, autos hapa hadharani
Pili aliwahi kutuambia kuwa Rais Sadam Husein alikuwa Rais wa Kuwait, hivi ni lini Sadam Hussein keshawahi kuwa Rais wa Kuwait??
Huyu jamaa ndiye angepaswa apigwe “ban” badala ya mtandao wetu wenye kusema ukweli wakati wote wa Jamii Forum