Halima Mdee....

Kwanza salamu sana ziwafikie wageni wetu kutoka jf ambao kwa mpaka sasa wameshajua kona na vichochoro vingi vya huu mtaa wa kt. Heshima kwenu natanguliza na naomba msamaha kama lugha au lafudhi hazitalingana sana katika uzi huu.
Naam, katika pitapita zangu za kurasa za habari nimejikuta sana na magazeti au kufwata wanasiasa wa bongo katika mitandao ya jamii. Kusema kweli, nilisifia sana jitihada za anko magu kabla wapambe wateke mada nzima kwa kutafuta kiki. Ila hio ni hadithi ya siku nyingine.
Katika wanasiasa walionivutia zaidi kwa bongo ni HALIMA MDEE, TUNDU LISSU, NAPE NAUYE NA MH.ZITTO KABWE. Hoja zao kuikosoa serikali na kuweka bayana yalio nyuma ya pazia ni mfano mzuri wa jinsi upinzani unavyotakiwa kuweka sawa na kuongelea pindi serikali iliyo mamlakani inapoleta longo longo za kiafrika.
Kabla sijapotelea zaidi kwenye mada iliyonileta hapa, halima mdee wakuu…Ni mrembo mwenye akili na shujaa. Kila kitu ninacho kiwaza na kutamani kiwe kwa mwanamke. Mheshimiwa akiwa anazungumza akili yangu inafunguka na kuwa makini zaidi alafu mawazo ya kutaka kumjua zaidi kiundani yananijia. Kama atakua anasoma habari hii huku ukimbizini ajue ustaarabu umeniishia na nimetokea kumpenda sana na kumuwaza nje ya maudhui au mantiki anayojulikana nayo ya kisiasa na kutetea jamii.

Mara nyingi japo najua ni mawazo ya kibwege nawaza tukiwa tumekaa nae kwenye mgahawa au pahali faragha tukijadili hoja tofauti tofauti na kuvutiwa na urembo na ucheshi wake. Kwa sasa hivi acha nipambane na hali yangu…kama wasemavyo waungwana…nikitumai ujumbe utamfikia mlengwa.

Uhuru wa kujieleza

unataka ugomvi na Ester bulaya?

Huko kwingine sawa, hapo kwenye sifa za urembo mhuuu!!!
Hata yeye anaweza kukukatalia.

yuko juu bana, na naona anaemkosoa kama adui vile!

kilio cha samaki hiki mwenzangu,naona machozi yanaenda na maji lkn haizuru

ni yupi huyo? na aje tu maana ndio kama hivo nishajieleza

Naomba kuwasilisha…
Asante
[ATTACH=full]179493[/ATTACH]

Ni kweli kuweka wazi yanayo sumbua mtima wako siyo jambo baya kabisa, ni kama mimi anavyo nikosha Dr Tulia kwa urembo wake na ile sauti hasa asemapo “swali la nyongeza!”

umeona eh? huyu yuko kwenye sala zangu baada ya kumuomba Mungu anipe afya njema

Ameshikilia moyo wako ilhali hajui wallah…

hapa nauza nyumba ya urithi na kama kuna ndugu ndani nawatimua wote wakatafute mchezo wakacheze…spendi upuzi mimi!!

Hapo ndipo ninapo wakubali wajaluo, mapenzi kwanza then pesa baadae… tehteehhh

Acha basi kusifia kituko kabisa acha niachie mbavu zangu mie… Juzi alikuw akwenye maonyesho ya mavazi akavaa vazi lenye suruali alikuwa kama mti umetundikwa khanga na mwenyewe analima… poor Tulia ni mbaya kuanzia sura mpk roho na meno yake kama Githeri yamesambaa mdomoni km mahindi ya kuchoma pale Uyole

Akiisoma hii post yako anaweza kujinyonga walahi!

Acha kuniumiza roho yangu mkuu Ngakumbuo! kipenda roho … aaahh Tulia! katuliza moyo wangu bibie!

mmmh yule sasa hivi hawezi maana anadhani dunia yote yake… nakwambia sikudanganyi nenda kaangalie utaona mwenyewe nikajiuliza mavazi yote alishindea hata kushona basi maksi tujue moja thou hatajulikana mbela wala nyuma lakini lingekuwa afadhali tuu sio kwa kituko kile cha suruali na gauni… Niacheni niko huku gikombaa natafuta raba na simple shoe jioni narudii zangu namanga

Picha picha picha ya Doctor kwenye gauni na suruali. Tafadhari

Ndio Ndio Hakika Ndio mwenyewe