Hakika Dini Zetu za Asili Zilikuwa na Nguvu.

Kabla ya ujio wa wageni kutoka Ulaya [Wazungu] na Mashariki ya Kati [Waarabu] jamii za watu Waafrika zilikuwa na dini pamoja na tamaduni zao bora na zenye nguvu.

Katika dini mbalimbali za Kiafrika ambazo huitwa na wageni pamoja na wafuasi wao kuwa matambiko na mizimu. Maombi fulani yalifanyika kwa lengo la ustawi katika jamii husika na maombi hayo yalijibiwa kwa wakati, kwa mfano kama wakiomba mvua basi zilinyesha kwa wakati.

Kwa kuwa sote tunaamini kuna Mungu mmoja mwenye Nguvu na vyote vilivyokuwepo vilivyopo na vijavyo ni kazi yake basi hata dini zetu za kale zilikuwa sahihi kabisa ila tu ni mapungufu ya kisayansi na kiteknolojia yalisababisha mafundisho yake yasiandikwe hivyo kupotea kwenye maandishi ila bado miiko yake na makatazo yake yako pale pale.

Kwa nini nasema dini zetu za asili zilikuwa na nguvu kuliko hizi za kisasa. Leo utakuta maelfu ya watu wanaoamini ama katika Ukristu au Uislamu kujitokeza kuomba jambo fulani lakini thubutu litokee kwa wakati ule. Lakini kwa dini zetu za Kiafrika ilikuwa punde tu mara baada ya maombi.

Kwa mfano hili la kufungiwa Jf ilikuwa ni jambo dogo tu, maombi ya wazee sita tu wenye utakaso mambo kisha na Jf ingerudi hewani wangetaka wasitake.

Au mnaonaje wanakijiji wenzangu?[ATTACH=full]179534[/ATTACH][ATTACH=full]179535[/ATTACH][ATTACH=full]179536[/ATTACH][ATTACH=full]179537[/ATTACH]

Mkuu hayo mambo mbona bado yapo? Hujaskia mtu kapigwa radi na kufa? Au wamezuia mvua isinyeshe! Ukweli watu wengi wana abudu zile dini za kale bila kujua.

Haaaaahaaaaa.Ngoja kwanza watu tutafute facts.

Hukupata kutambua ya kuwa dini ni Imani ya kile unachokiamini? Nani basi mwenye uwezo wa kutambua dini ya kweli yu ngali katika umbo la nyama lililo la kibinadamu?

Ni kweli.

Hmm!..

Zile za kale hazikua dini… yale yalikua matambiko na nguvu za giza…

Cc: @Mahondaw

Kwa hakika zilikua dini na pia zilikua na misingi yake ya namna ya kumuomba Mungu na zilikua na maonyo, makatazo, miongozo pamoja na ahadi njema kama zilivyo hizi za Wazungu na Waarabu.

Nimekumbuka miaka hiyoooo olevo kwenye song of lawino and ocol juu ya ATR

cc @Smart911

sure na hazina tofaut sana na hizi za sasa bt tulishindwa tu jinsi ya kuziweka kwenye maandishi na kuzisambaza kama hao wazungu na waarabu

Umekumbukae, wote Lawino na Ocol walikua na hoja sawa katika kutetea dini zao. Mmoja akitetea ile ya asili na mwingine ile ya kizungu.

Umeonae, wazee wetu walimjua Mungu kupitia dini zao za mwanzo na ndiyo maana neno linalosimama kwa ajili ya jina la Mungu/Allah lipo karibu katika viluga vya makabila yote.

Uliwahi kushuhudia mvua haijanyesha na ukame ukatesa watu hadi wazee wa kijiji wakaitana kwa dharura kufanya maombi chini ya mti au ndani ya msitu mnene!!!

Dini tumeletewa tu ila maombi ya kuabudu yalifanyika na mungu alisikiliza haraka sana

yeah ila lawino alikuwa na logic sana yule mwanamke kwa matusi sasa mweh!!!

cc @Smart911

Kweli kabisa

Lawino

tatizo akina watu wabishi sana, wanaogopa sijui, Mshana jr sikia hii au nawe ushaokoka

Zilituletea Umaskini mkubwa