Hakika Dini Zetu za Asili Zilikuwa na Nguvu.

Chimgege

Senior Villager
#1
Kabla ya ujio wa wageni kutoka Ulaya [Wazungu] na Mashariki ya Kati [Waarabu] jamii za watu Waafrika zilikuwa na dini pamoja na tamaduni zao bora na zenye nguvu.

Katika dini mbalimbali za Kiafrika ambazo huitwa na wageni pamoja na wafuasi wao kuwa matambiko na mizimu. Maombi fulani yalifanyika kwa lengo la ustawi katika jamii husika na maombi hayo yalijibiwa kwa wakati, kwa mfano kama wakiomba mvua basi zilinyesha kwa wakati.

Kwa kuwa sote tunaamini kuna Mungu mmoja mwenye Nguvu na vyote vilivyokuwepo vilivyopo na vijavyo ni kazi yake basi hata dini zetu za kale zilikuwa sahihi kabisa ila tu ni mapungufu ya kisayansi na kiteknolojia yalisababisha mafundisho yake yasiandikwe hivyo kupotea kwenye maandishi ila bado miiko yake na makatazo yake yako pale pale.

Kwa nini nasema dini zetu za asili zilikuwa na nguvu kuliko hizi za kisasa. Leo utakuta maelfu ya watu wanaoamini ama katika Ukristu au Uislamu kujitokeza kuomba jambo fulani lakini thubutu litokee kwa wakati ule. Lakini kwa dini zetu za Kiafrika ilikuwa punde tu mara baada ya maombi.

Kwa mfano hili la kufungiwa Jf ilikuwa ni jambo dogo tu, maombi ya wazee sita tu wenye utakaso mambo kisha na Jf ingerudi hewani wangetaka wasitake.

Au mnaonaje wanakijiji wenzangu? wp_ss_20180625_0001 (2).png wp_ss_20180625_0004 (2).png wp_ss_20180625_0005 (2).png wp_ss_20180625_0002 (2).png
 
#2
Mkuu hayo mambo mbona bado yapo? Hujaskia mtu kapigwa radi na kufa? Au wamezuia mvua isinyeshe! Ukweli watu wengi wana abudu zile dini za kale bila kujua.
 

Tatigha

Senior Villager
#4
Hukupata kutambua ya kuwa dini ni Imani ya kile unachokiamini? Nani basi mwenye uwezo wa kutambua dini ya kweli yu ngali katika umbo la nyama lililo la kibinadamu?
 

park don

Village Elder
#10
sure na hazina tofaut sana na hizi za sasa bt tulishindwa tu jinsi ya kuziweka kwenye maandishi na kuzisambaza kama hao wazungu na waarabu
 

Join Chatpanda, Fastest growing social media website in Kenya! Get verified easily, grow your following, and meet like-minded Kenyans

Chimgege

Senior Villager
#12
sure na hazina tofaut sana na hizi za sasa bt tulishindwa tu jinsi ya kuziweka kwenye maandishi na kuzisambaza kama hao wazungu na waarabu
Umeonae, wazee wetu walimjua Mungu kupitia dini zao za mwanzo na ndiyo maana neno linalosimama kwa ajili ya jina la Mungu/Allah lipo karibu katika viluga vya makabila yote.
 

Join Chatpanda, Fastest growing social media website in Kenya! Get verified easily, grow your following, and meet like-minded Kenyans


Join Chatpanda, Fastest growing social media website in Kenya! Get verified easily, grow your following, and meet like-minded Kenyans

Top