Katika hali isiyotegemewa msanii maarufu Duniani na Afrika nzima Diamond Platnumz ametoa sapraizi ya aina yake baada ya kuibuka kwenye show iliyoandaliwa na Clouds Media na kushea stage moja na mkali kutoka Nigeria Davido,wasanii hao wawili waliimba wimbo wao wa Number one remix huku wakikonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye ukumbi wa Next door Arena Masaki jijini Dar.
Kabla ya kufika mahali hapo pia Diamond alitoa sapraizi nyingine kwenye usiku wa Kusi,show iliyofanyika Dar Live Mbagala na kuimba kwa pamoja na msanii anayetamba kwa sasa kutoka WCB harmonize ambapo waliperfom vibao kama Ngoja na Kwangwaru.
Mpaka nawaletea habari hii gumzo limebaki huko mitandaoni na mijadala mikali kwamba huenda huu ndio ukawa mwanzo wa tamati ya mgogoro uliopo kati ya WCB na Clouds Media huku mashabiki wengine wakisema huenda Clouds chini ya Kusaga wameamua kumuita Diamond kumuonyesha wao hawana tatizo naye isipokuwa bwana Ruge ambaye anaumwa hoi bin taaban na hayuko bongo mwezi mzima sasa ndiye mwenye chuki zake binafsi.
Toa Maoni Yako.
Habari na @chinga one wa JF kwa sasa mkimbizi nchini Kenya Count ya Madhare ndani ya Kenya Talk.
[ATTACH=full]176701[/ATTACH][ATTACH=full]176702[/ATTACH]