Faida za embe ng'ong'o kiafya

Unaweza usielewe pale mtu anaposema nataka kula embe Sakua, wengi wetu tumezoea kuliita ‘embe ng’ong’o’.

Tunda hili ni miongoni mwa yenye viini lishe na vitamini A, C, beta carotene, madini ya potassium na magineziamu.

Mbali ya tunda hilo kuwa na viini lishe, pia linakiasi cha sukari ya asili aina ya fructose na glucose ambazo huupatia mwili nguvu.

Ulaji wa maembe ng’ong’o mara kwa mara unaweza kukuepusha kupata vidonda vya koo kwa sababu tunda hilo lina vijiua sumu.

Kwa mujibu wa Jarida la Asian Pacific of Tropical Biomedicine lililochapishwa mwaka 2013, linasema sharubati (juisi) ya embe ng’ong’o huongeza hamu ya chakula kutokana na uwezo wake wa kusisimua vitu vya maonjo katika ulimi.

Moja ya faida za tunda hili husaidia kupunguza hatari ya kupata saratani.

Pia ulaji wa embe hilo mara kwa mara husaidia damu isigande kwenye mishipa.

Unywaji wa sharubati ya tunda hilo hupunguza pia uwezekano wa mtu kupata unene wa mwili wa kutisha na kuwa ni kero.

Hivyo, inashauriwa, familia zitumie zaidi tunda hilo kwa ajili ya kujenga afya na kuzuia baadhi yamaradhi kama hayo ya saratani kama inavyoelekezwa na wataalamu wa tiba lishe.

tukumbuke si kila ugonjwa unaweza kutibiwa na dawa za hospitali tu, bali hata vyakula na matunda ni tiba tosha.

Unaposema Embe Ng’ong’o unanikumbusha na mabungo! Sijui kama bado mabungo yanapatikana kwa wingi kama enzi zile za miaka ya sabini na themanini huko Dar!

Haya nakumbuka shambani kwetu kimara yalikuwa mengi sana,siku hizi sio tena mashamba ni makazi ya watu kwahiyo hayapo kabisa labda maeneo ya Kisarawe…

Nguvu za kiume vipi?

Duh!

huku kwetu wanaita embe nyonyo

Nadhani embe nyonyo ni zile ndogo za kunyonya zikiwa zimeiva, embe ng’ong’o zenyewe kokwa lake lina miba

Ahaa bas me ndo nmeshindwa kutofautisha

Weka na picha la hiyo embu…

Cc: @Mahondaw

Hahahahaha… Smart naomba ukija unijie na maembe ng’ongo

Ndio yapoje hayo?

Duh

Kwan ww huna nguvu??

ninazo mkuu

So what for???

kuitumia hiyo nguvu tuu

kama nyonyo

Aisee basi yatakua mazuri sana

yeah

Wanikumbusha Ndanda Masasi.