Comrade wangu Mbunge John Heche katika hili la Peter Zacharia nakukatalia na acha Siasa na Ukabila tafadhali

[FONT=courier new]Nianze Kwanza kwa kuweka wazi kwamba Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche ni Rafiki yangu sana tu ( wenyewe mliosoma na kuelimika mnaita Comrade ) na Urafiki wangu nae haujaanzia hapa alipokuwa Mheshimiwa Mbunge bali ameanza kuwa Rafiki yangu tokea tulipokuwa Masomoni SAUT Yeye akifanya Kozi yake ya Ualimu nami ya Mawasiliano na tulikuwa tukishirikiana kwa mambo mbalimbali ya Kitaaluma na Kijamii pale Nsumba na Malimbe takribani miaka kama Kenda / Tisa imepita sasa.

Huko nyuma wakati tukiwa bado Nyumbani kunako ( JamiiForums ) nilishawahi siku moja kuanzisha ’ Uzi ’ maalum kabisa wa Kumsifia na Kumkubali sana Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche hasa kutokana na nilivyomjua na kushirikiana nae katika mambo mbalimbali kabla hajaingia Siasani na mpaka leo au hivi sasa natiririka na naserereka na huu ’ Uzi ’ bado atabaki kuwa mmoja wa Watu ambao GENTAMYCINE Mimi nawakubali japo Yeye ni Mpinzani na Mimi ni Chama Tawala.

Pamoja na Sifa / Kongole zangu zote hizo Kwake ’ Comrade ’ wangu Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche leo bila ya kupepesa macho, kumung’unya maneno na kutikisa masikio yangu najitoa muhanga ( najilipua ) katika ’ Kumchana ’ au kumpa ’ makavu ’ yangu Comrade wangu huyu hasa juu ya tabia ambazo kwa Siku za karibuni naona amekuwa nazo na kinachoniuma huko nyuma kote ambako nilibahatika kuwa nae hakuwa na hizi tabia na sijui amekubwa na nini.

Comrade wangu Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche nimepitia ukurasa wako wa ’ Twitter ’ muda si mrefu na kuona umeandika kwamba umeshtushwa sana kama siyo mno na ’ tukio ’ zima lililomtokea jana ’ Mkurya ’ mwenzako Mfanyabiashara Peter Zacharia ambaye pia ni Mwana CCM ’ lia lia ’ kama siyo ’ kindaki kindaki ’ kabisa huku ukisema kwamba unaomba ukweli uwekwe wazi haraka juu ya suala / jambo lenyewe na kwamba muda si mrefu wana Tarime kupitia Wewe Mbunge wao utalitolea ufafanuzi mkali kana kwamba mwenzetu Wewe ambaye ni kwa bahati nzuri ni mwana CHADEMA ’ kindaki kindaki ’ kama siyo ’ lia lia ’ unaujua ukweli wote.

Comrade wangu Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche Mimi leo nakuomba na nakusihi kabisa kwamba acha sana kupenda kuwa ’ Political Opportunist ’ na ’ Mkabila ’ uliyepitiliza kwani unaweza kudhani haya yanakujenga zaidi ila kwa Jicho la ’ Kiumakini ’ kabisa ’ tuliobarikiwa ’ kidogo kuona mbali tunaona kuwa ’ unajiharibia ’ na ’ unaharibu ’ pia vile vile. Nikuombe tu kwamba ’ Ukada ’ wako uliotawaliwa na ’ Uanaharakati ’ usikubadili na leo hii Mimi Comrade wako GENTAMYCINE wa SAUT yetu ile ya Fr. Dr. Kitime nikakuona ni wa tofauti badala yake simamia ukweli na usipende ’ Kujidhatiti ’ Kisiasa kwa kutumia ’ migongo ’ ya Watu wengi wenye ’ Uvivu ’ wa Kufikiri na Kuchanganua mambo kwa Kina.

Sipo hapa katika Kumuhukumu ’ Poti ’ wangu Mfanyabiashara Peter Zacharia na hasa nikiamini kabisa kwamba sina uhakika wa nini kimemtokea, chanzo chake ni nini na kitu gani labda kimepelekea Yeye kufanya tunayoaminishwa kwamba ameyafanya na nao Watu waliojeruhiwa nae ( ambao bado siwajui na sidhani kama pia nina uwezo wa kuwajua ) ila nina uhakika kabisa tena wa 100% kuwa Comrade wangu Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche na hata wana Tarime hasa wale wasiopenda ’ Unafiki ’ wanajua kabisa tabia ’ chafu ’ alizonazo na ambazo pia sidhani kama ’ Tajiri ’ Peter Zacharia kuna siku atakuja kuziacha.

Leo sitaki niziweke hapa hizo tabia zake ila labda nitakuacha tu na maswali yangu kadhaa Kwako kwamba unadhani ni kwanini jana baada ya kumpata yaliyompata karibia 75% ya Wana Tarime, Wana Mkoa wa Mara na Mkoa jirani wa Mwanza walifurahi sana? Je Mbunge na Comrade wangu John Heche unadhani leo hii ile Familia ya yule Ndugu ambaye alimwagiwa ’ Tindikali ’ tena kwa ’ makusudi ’ kabisa na ’ Poti ’ Peter Zacharia itamshukuru Mwenyezi Mungu au itachukia? Je Comrade Watu wakihisi kwamba umeamua kulivalia ’ njuga / kibwaya ’ hili jambo kwakuwa hakuna asiyejua kuwa Wewe na Yeye ( Mkamatwaji PZ ) ni ’ Maswahiba ’ wakubwa tu na kuna hata ’ Financial Favors ’ unazipata kutoka Kwake japo Wewe ni mwana CHADEMA watakuwa wamekosea? Ninayo mengi Comrade ila nadhani kwa kuanzia tu kwa leo nianze na haya.

Hata hivyo pamoja na kwamba nimeandika yote haya Kwako ila kaa ukijua kwamba Mimi GENTAMYCINE ’ [COLOR=rgb(184, 49, 47)]Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer ’ nakukubali na napenda sana ’ Spirit ’ yako hasa ya Uwajibikaji na ya Kisiasa na niseme tu kwamba kama kuna ’ Jembe ’ ambalo CHADEMA wamelipata na wanatakiwa kulitunza ni Wewe Comrade wangu Mheshimiwa Mbunge wa Tarime ’ Poti ’ John Heche.

Na nimalizie tu kwa ’ kumchombezea ’ kidogo tu Mfanyabiashara na Tajiri Peter Zacharia kwamba siku zote malipo huwa ni hapa hapa duniani halafu Pesa huwa siyo kila kitu katika maisha ya Mwanadamu na akumbuke kama pia siyo kutambua kwamba kila awamu huwa na Kitabu chake. Naomba niibe tu neno la Kiingereza lisemalo ’ What goes around comes around ’ [COLOR=rgb(184, 49, 47)]Naomba niishie hapa tafadhali.

Nawasilisha.[/FONT]

meneno mengi halafu yote porojo. jinga kabisa wewe mleta mada. popoma mkubwa wee.

Nadhani CDM wawe makini sana na Migogoro ya CCM

Nilisha mshauri awahi tiba ya afya ya akili kabla mambo hayaja haribika kabisa hakunielewa. Haya, asiye fichua ugonjwa wake kilio (kuvua nguo) kitamuumbua

Nakuunga mkono.

Walioelewa tusaidieni kudadavua.

Sijaona kosa la Heche labda wachangiaji wengine wataliona

ngoja ntulie ntajua mengi yaliyojificha aseee,endeleen kuanikana tu tujue zaid

:meffi::meffi:

Wewe mpuuzi si ulisema we ni Mnyarwanda? Sasa CCM ipo hadi huko au vipi? Acha uongo unaumbuka sasa.

Ngoja nirudie tena kuusoma uzi wako.

Cc @Mfiaukweli @Luambo Makiadi @kyekomakubi @MENGELENI KWETU njooni tujadili mada huku

Sioni kibaya alichozungumza Heche. Yeye alichohoji ni mbinu iliyotumika. Mbinu hiyo haina tofauti na zile zinazotumika kunyamazisha watu wasio na hatia. Ni kweli Zacharia ni mchafu, kwanini asikamatwe na polisi kwa njia za kawaida , badala ya watu waliovaa kiraia tena usiku?

Hiyo mbinu ya watu wasijulikana sio nzuri kwa sasa. Kwani kulikuwa na shida gani hao usalama wa taifa wangeandamana na polisi kwenda kumkamata kisha kutumia taratibu za ndani kumuhoji watakacho?

afadhali mmeliona popoma

Umehudhuria shule tu lakini hujaelimika wewe popoma.

Zakayo aliona ajihami mapema na mitutu ya bunduki maana angepotezwa
Safi sana Zaka

Umejidhihirisha ulivyo malaya na mnafiki! Mara mnyarwanda mara mwana ccm! PUMBAVU!
SHITHOLE!!

Narudi

Mkuu hakuna cha kujadili hapo…
Mwanzo wa uzi mpaka mwisho ni UPUUZI MTUPU…

Huwezi kuelewa kitu hapo Mkuu.