Comrade wangu Mbunge John Heche katika hili la Peter Zacharia nakukatalia na acha Siasa na Ukabila tafadhali

Tindo

Village Elder
#21
Nianze Kwanza kwa kuweka wazi kwamba Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche ni Rafiki yangu sana tu ( wenyewe mliosoma na kuelimika mnaita Comrade ) na Urafiki wangu nae haujaanzia hapa alipokuwa Mheshimiwa Mbunge bali ameanza kuwa Rafiki yangu tokea tulipokuwa Masomoni SAUT Yeye akifanya Kozi yake ya Ualimu nami ya Mawasiliano na tulikuwa tukishirikiana kwa mambo mbalimbali ya Kitaaluma na Kijamii pale Nsumba na Malimbe takribani miaka kama Kenda / Tisa imepita sasa.

Huko nyuma wakati tukiwa bado Nyumbani kunako ( JamiiForums ) nilishawahi siku moja kuanzisha ' Uzi ' maalum kabisa wa Kumsifia na Kumkubali sana Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche hasa kutokana na nilivyomjua na kushirikiana nae katika mambo mbalimbali kabla hajaingia Siasani na mpaka leo au hivi sasa natiririka na naserereka na huu ' Uzi ' bado atabaki kuwa mmoja wa Watu ambao GENTAMYCINE Mimi nawakubali japo Yeye ni Mpinzani na Mimi ni Chama Tawala.

Pamoja na Sifa / Kongole zangu zote hizo Kwake ' Comrade ' wangu Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche leo bila ya kupepesa macho, kumung'unya maneno na kutikisa masikio yangu najitoa muhanga ( najilipua ) katika ' Kumchana ' au kumpa ' makavu ' yangu Comrade wangu huyu hasa juu ya tabia ambazo kwa Siku za karibuni naona amekuwa nazo na kinachoniuma huko nyuma kote ambako nilibahatika kuwa nae hakuwa na hizi tabia na sijui amekubwa na nini.

Comrade wangu Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche nimepitia ukurasa wako wa ' Twitter ' muda si mrefu na kuona umeandika kwamba umeshtushwa sana kama siyo mno na ' tukio ' zima lililomtokea jana ' Mkurya ' mwenzako Mfanyabiashara Peter Zacharia ambaye pia ni Mwana CCM ' lia lia ' kama siyo ' kindaki kindaki ' kabisa huku ukisema kwamba unaomba ukweli uwekwe wazi haraka juu ya suala / jambo lenyewe na kwamba muda si mrefu wana Tarime kupitia Wewe Mbunge wao utalitolea ufafanuzi mkali kana kwamba mwenzetu Wewe ambaye ni kwa bahati nzuri ni mwana CHADEMA ' kindaki kindaki ' kama siyo ' lia lia ' unaujua ukweli wote.

Comrade wangu Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche Mimi leo nakuomba na nakusihi kabisa kwamba acha sana kupenda kuwa ' Political Opportunist ' na ' Mkabila ' uliyepitiliza kwani unaweza kudhani haya yanakujenga zaidi ila kwa Jicho la ' Kiumakini ' kabisa ' tuliobarikiwa ' kidogo kuona mbali tunaona kuwa ' unajiharibia ' na ' unaharibu ' pia vile vile. Nikuombe tu kwamba ' Ukada ' wako uliotawaliwa na ' Uanaharakati ' usikubadili na leo hii Mimi Comrade wako GENTAMYCINE wa SAUT yetu ile ya Fr. Dr. Kitime nikakuona ni wa tofauti badala yake simamia ukweli na usipende ' Kujidhatiti ' Kisiasa kwa kutumia ' migongo ' ya Watu wengi wenye ' Uvivu ' wa Kufikiri na Kuchanganua mambo kwa Kina.

Sipo hapa katika Kumuhukumu ' Poti ' wangu Mfanyabiashara Peter Zacharia na hasa nikiamini kabisa kwamba sina uhakika wa nini kimemtokea, chanzo chake ni nini na kitu gani labda kimepelekea Yeye kufanya tunayoaminishwa kwamba ameyafanya na nao Watu waliojeruhiwa nae ( ambao bado siwajui na sidhani kama pia nina uwezo wa kuwajua ) ila nina uhakika kabisa tena wa 100% kuwa Comrade wangu Mheshimiwa Mbunge wa Tarime John Heche na hata wana Tarime hasa wale wasiopenda ' Unafiki ' wanajua kabisa tabia ' chafu ' alizonazo na ambazo pia sidhani kama ' Tajiri ' Peter Zacharia kuna siku atakuja kuziacha.

Leo sitaki niziweke hapa hizo tabia zake ila labda nitakuacha tu na maswali yangu kadhaa Kwako kwamba unadhani ni kwanini jana baada ya kumpata yaliyompata karibia 75% ya Wana Tarime, Wana Mkoa wa Mara na Mkoa jirani wa Mwanza walifurahi sana? Je Mbunge na Comrade wangu John Heche unadhani leo hii ile Familia ya yule Ndugu ambaye alimwagiwa ' Tindikali ' tena kwa ' makusudi ' kabisa na ' Poti ' Peter Zacharia itamshukuru Mwenyezi Mungu au itachukia? Je Comrade Watu wakihisi kwamba umeamua kulivalia ' njuga / kibwaya ' hili jambo kwakuwa hakuna asiyejua kuwa Wewe na Yeye ( Mkamatwaji PZ ) ni ' Maswahiba ' wakubwa tu na kuna hata ' Financial Favors ' unazipata kutoka Kwake japo Wewe ni mwana CHADEMA watakuwa wamekosea? Ninayo mengi Comrade ila nadhani kwa kuanzia tu kwa leo nianze na haya.

Hata hivyo pamoja na kwamba nimeandika yote haya Kwako ila kaa ukijua kwamba Mimi GENTAMYCINE ' Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer ' nakukubali na napenda sana ' Spirit ' yako hasa ya Uwajibikaji na ya Kisiasa na niseme tu kwamba kama kuna ' Jembe ' ambalo CHADEMA wamelipata na wanatakiwa kulitunza ni Wewe Comrade wangu Mheshimiwa Mbunge wa Tarime ' Poti ' John Heche.

Na nimalizie tu kwa ' kumchombezea ' kidogo tu Mfanyabiashara na Tajiri Peter Zacharia kwamba siku zote malipo huwa ni hapa hapa duniani halafu Pesa huwa siyo kila kitu katika maisha ya Mwanadamu na akumbuke kama pia siyo kutambua kwamba kila awamu huwa na Kitabu chake. Naomba niibe tu neno la Kiingereza lisemalo ' What goes around comes around ' Naomba niishie hapa tafadhali.

Nawasilisha.
Wakiendelea kutandikwa risasi hivihivi, lile kundi la wasiojulikana litajitokeza na tutawatambua washirika wao hata humu mitandaoni.
 
Stroke

Senior Villager
#22
Kwa hili bandiko nimehutimisha kuwa kila mtu ana bei yake;

Hata zile Kelele zote za Lisu mpaka mapovu yanamtoka mdomoni hazikuwa bure..
 
#27
Wengi nimegundua mnachuki binafsi na huyu POPOMA,C.FELA kiasi kwamba akiweka hoja yeyote mnakimbilia kutukana pengine bila hata kusoma alichoandika
Punguzeni mihemko waungwana na kama tupo hivi raia wa Tanzania basi acheni tuendlee kuporwa pesa za korosho.

Kifupi Tarime nzima inashangilia tukio hili pengine la kihistoria kwao.

Zakaria ni zaidi ya Zakaria wa mabasi achana na dharau zake ni zaidi ya hayo

Usalama acheni wafanye kazi yao na hayo ni matukio yanayowakuta katika kazi na wanastahili kumfuata zakaria

Wiki jana Zakaria alienda kanisani kutubu na kuomba waumini wamwombee maana usalama wako nyuma yake......Mke wake yupo rupango kwa makosa kadhaa....

Polisi Tarime au Mara kiujumla ipo mikononi mwake na sometime huwa anawapiga hadi makofi,......

Inshu hii ni pana sana aisee wala wanasiasa wasiichukulie kama ndio kigezo cha kuidharau TISS.

UWT wanajua wafanyacho tusifikie hatua ya kuwadharau kiasi hicho.

Dodoso tu ni kuwa inshu hii inaanzia kwa Tajiri wa supa Sami kisha Nyanza..................Acheni uzwazwa na msipende kumshambulia POPOMA wa kale kwa kudhani hajui alichoandika.
 
#29
Kwa hizi kombora alizopewa mleta mada atakuwa anauchungulia huu uzi namna hii.
hii ndio kenyatalk bhana... full freedom. hakuna kuogopana wala kuleteana unafiki na kusifiana ujinga kama kule jf.

nimependa moderator wa huku wanavyotuacha tunyoshane wenyewe kwa wenyewe. hakuna ban za kijinga, kufuta post au kuunganisha thread.
 
Last edited:
#30
Wengi nimegundua mnachuki binafsi na huyu POPOMA,C.FELA kiasi kwamba akiweka hoja yeyote mnakimbilia kutukana pengine bila hata kusoma alichoandika
Punguzeni mihemko waungwana na kama tupo hivi raia wa Tanzania basi acheni tuendlee kuporwa pesa za korosho.

Kifupi Tarime nzima inashangilia tukio hili pengine la kihistoria kwao.

Zakaria ni zaidi ya Zakaria wa mabasi achana na dharau zake ni zaidi ya hayo

Usalama acheni wafanye kazi yao na hayo ni matukio yanayowakuta katika kazi na wanastahili kumfuata zakaria

Wiki jana Zakaria alienda kanisani kutubu na kuomba waumini wamwombee maana usalama wako nyuma yake......Mke wake yupo rupango kwa makosa kadhaa....

Polisi Tarime au Mara kiujumla ipo mikononi mwake na sometime huwa anawapiga hadi makofi,......

Inshu hii ni pana sana aisee wala wanasiasa wasiichukulie kama ndio kigezo cha kuidharau TISS.

UWT wanajua wafanyacho tusifikie hatua ya kuwadharau kiasi hicho.

Dodoso tu ni kuwa inshu hii inaanzia kwa Tajiri wa supa Sami kisha Nyanza..................Acheni uzwazwa na msipende kumshambulia POPOMA wa kale kwa kudhani hajui alichoandika.
naona umeamua kurudi na ki ID chako kingine cha dharula. utapata tabu sana.
popoma wahed.
 
Mfiaukweli

Village Elder
#31

Hapo kwenye bold; ndio hoja ya wengi wetu (tusiokubali kushangilia ujinga). Kama kweli UWT wanajua walifanyalo, (Zakaria hajaanza hayo anayotuhumiwa kuyafanya jana alipokamatwa - na kama ulivyotutanabahisha hapa Polisi wapo mikononi mwake na sometimes huwa anawapiga hadi makofi) NI KWA NINI WASIMCHUKULIE HATUA SIKU ZOTE HIZO - hadi wamchukulie hatua jana???? Huyu bwana magari yake ndio yalikuwa yanatumika kusomba watu kwenda kwenye mikutano ya kampeni ya ccm - halafu mara nyingi baada ya mikutano usafiri wa kurudi nyumbani "unajiju" - kipindi hicho alikuwa msafi??

Kwa nini tusiamini kuwa kuna kitu kingine nyuma ya pazia kilicholeteleza yote haya? Mwenye majibu ya kueleweka juu ya mashaka yangu haya na aje aniambie.
 
#34

Nadhani unaelewa nini maana ya pesa katika awamu zilizopita lakini pia ni kama nilivyosema inshu hii ni pana sana.

Ziara ya PM ndio chanzo cha yote Chief hadi mkewe sasa yupo selo karibu mwezi mzima sasa.

Lakini pia kifo cha tajiri mwenzie Super Sami......
Let's end this diskasheni Chiefs yasio tuhusu tuyaache kidogo tijadili yenye tija zaidi kwetu sote
 
Elungata

Village Elder
#38
Hahahaha,rafiki yangu @getamycine naona bora urudi nyumbani huku kumekukataa,Kule watu walikuwa wanaogopa ban,
Huku utayaoga matusi had I basi
 
#39

Sijutii na tena kwa taarifa yako kwakuwa Mimi ndiyo Makao Makuu ya hayo ' Matusi ' na maneno yote ya ' Shombo ' unayoyajua na hata yale usiyoyajua huku sasa ndiyo napapenda kwani nitaweza kuwaonyesha dhahiri kuwa sina ' Mshindani ' na huku sasa ndiyo ' watayakoga ' hadi wajute kuifahamu hii ' Brand ID '.

Kama wakati wa Kampeni za Urais mwaka 2015 nilikuwa ' Mwiba Mchungu ' kwa Wapinzani na hasa wana CHADEMA tena waliokuwa wengi kule Nyumbani JamiiForums kuliko hata hapa ' Ukimbizini ' Kenya Talk ndiyo unadhani wataniweza?

Halafu uzuri ni kwamba nimetokea katika ' Makabila ' mawili hatari, muhimu na makini ya Zanaki na Tutsi hivyo Kwetu Sisi ' Kuogopa ' chochote au lolote ni ' mwiko ' na moja ya ' Sifa ' yetu kubwa ni kupenda Vita, Mapambano na Hatari hivyo nayatendea haki yote hayo.

' Principle ' yangu itabaki ni ile ile milele niwapo humu Mitandaoni kwamba ukija Kistaarabu basi utampenda GENTAMYCINE ila ukija ' Kishari ' utajuta kunifahamu kwani nitakushughulikia kwa mbinu zangu zote na hakuna Vita ninayoipenda na kuimudu vilivyo kama ya ' Kisaikolojia '.

Kama kawaida Wewe ' Ukijamba ' tu basi Mimi ' naharisha ' kabisa na namalizia na ule msemo wa Rais wa Uganda Mzee Yoweri Kaguta Amos Museveni anaosema naunukuu...." I pay You according to your Price ". Na Wewe kama unajisikia pia Kuungana na hao ' Wapumbavu ' katika ' Kupambana ' na Mimi ruksa tu kwani huwa napenda sana ' Kushambuliana ' na Idadi kubwa ya Watu kwakuwa nina ' Jeuri ' ya Kuwamudu na hawana ' ubavu ' wa kuniweza.

Nimemaliza.
 
#40

wee choko tu.
 
Top