CHURA!

slim5

Village Elder
#1
JIFUNZE KWA CHURA

Ukimchukua chura ukamuweka kwenye sufuria la maji kisha ukatenga motoni, kitakachotokea ni kwamba kadli maji yanavyozidi kupata joto chura naye anakuwa na uwezo wa kujiongeza joto la mwili wake. Chura atazidi kutumia nguvu zake kuuongeza mwili wake joto ili kuendana na joto la maji.

Lakini itafika wakati maji yatakapokuwa yanakaribia kuchemka chura atakuwa hana tena uwezo wa kuendelea kujiongeza. Wakati huu chura atafanya maamuzi ya kuruka na kutoka nje ya sufulia ili walau kutetea maisha yake.

Ataruka na kuruka lakini hatafanikiwa kwa sababu atakuwa ameshapoteza nguvu nyingi wakati alipokuwa akijiongeza ili kuendana na joto la maji. Baadaye maji yatachemka na punde tu chura atakufa.

Swali ni Je! Kitu gani kitakuwa kimemuua chura? Wengi watasema maji ya moto ndiyo yaliyo muua chura. Lakini kwa mtazamo wangu ni kwamba kilichomuua chura ni ujinga wake mwenyewe na kushindwa kuamua ni wakati gani sahihi wa kuruka.

Kijana mwenzangu, hebu fanya maamuzi sahihi sasa. Ruka ungali una nguvu zako zote usisubiri mpaka hali iwe mbaya. Ni kweli maisha tuliyonayo yanahitaji kujiongeza kwa kiasi kikubwa sana, lakini angalia usiwe kama chura wa kwenye tungo hii.

Hapa ninachomaanisha ni kwamba hautakiwi kung'ang'ana na jambo moja kwa muda mrefu kiasi cha kupoteza muda wako pasi na manufaa yoyote. Mwisho ukajikuta umepotea kabisa kwenye ramani ya maisha.

Unapaswa utambue kwamba katika maisha kila mtu ana mlango wake wa kutokea, hivyo ni vigumu sana kutoka kupitia mlango ambao hujaandikiwa.

Kazi ya control C na control P.
 

Top