Chapat za kusukuma

Chapat za kusukuma ni janga au changamoto kwa wanawake/wasichana walio wengi

Chapat za kusukuma ni kuukanda unga vizuri had yale mabonge bonge yasiwepo yan unga uwe smooth pia usiubwabwarize maji yan usiuzidishe maji uwe mtepe wengine wamekremisha chapat had uzichemshie maji

Mimi hua nafanya had za maji baridi na zinakua laini

Hata hivo chapat usizinyime mafuta yasiwe mengi had yajifyonze kiasi tu yanatosha kwenye kukunjia chapat had kuzikaanga kwenye chuma chake[ATTACH=full]178031[/ATTACH]

Tufundishe njia mbalimbali za kuchoma nyama…kuanzia kitimoto,ya ng’ombe,mbuzi na nyamapori bila kusahau ule mchanyiko wangu pendwa Bomba aka Mtura.

Ukinambia kuhusu kiti moto utakua unanoonea bure hata hiyo mitura sjwah kuila kabisa

Samahani sikujua naongea na mpishi tokea Mombasa…hadi nikatamka kitu haramu…
Hapa ngoja nisepe taratiiiibu.

Sitokei mombasa bwana lakini me muslim hiyi kiti moto kwangu no

Nazipenda sana hizi,hasa kama unaambatanisha mezani na supu ya utumbo au kuku…

Upate laini zenye ngozi tatu utapenda kila siku upikiwe

Kuandaa mtura
Chukua utumbo ule mkubwa wa mbuzi au ng’ombe usafishe vizuri.
Katakata nyama vipande vidogo vidogo sana, katakata vitunguu carrots na hoho (shape ya square).
Changanya vipande vya nyama na hivo viungo (Carrot hoho na vitunguu) na chumvi kisha weka katika ule utumbo mkubwa, funga utumbo ili visimwagike choma na moto kiasi, vitadondosha maji hadi vikauke.

Inaonesha vitam japo sjawah kuvila

Asante sana Evelyn salt…ntajaribu…ila naona ishu ni kuupata huo utumbo.

ni mtamu kwakweli kwa Arusha pale Kenny garden ukifika mlangoni utasalivate.
Dar nishapata mara moja pale kumekucha kwenye mbuzi mtura pia unapatikana.
home made mara moja moja

Utumbo ukienda buchani utapata ila kama upo karibia na machinjioni unauibukia huko huko

Changamoto za chapati:
Kuwa ngumu
kuwa shapeless

Ili chapati zisiwe ngumu:

Kanda unga kwa muda mrefu hadi uwe laini, uchanganyikane vizuri. Uunga uliokandwa vizuri muda wa kusukuma huwa unatokea vi bubbles (unajaa kama vile unavopuliza big G ) hapo ujue unga upo vizuri.

Wakati wa kukanda usiweke maji mengi hadi unga uwe mtepe kisha uanze kuongeza ongeza unga kuufanya uwe mgumu, chapati zitakua ngumu.
Weka maji au kimiminika kidogo kidogo hadi kitoshee

Wakati wa kukaanga chapati, usikaange na moto mdogo sana.

kutengeneza shape ya duara hapo ufundi sasa :smiley:

Jinsi ya kupika chapati nzuri (recipe ya Evelyn Salt)

Ngano
Maziwa ya unga
Maji (moto baridi yote sawa)
Chumvi

Weka ngano kwenye chombo
weka maziwa ya unga
chumvi kiasi kisha changanya
weka maji anza kukanda unga hadi ulainike vizuri (usiwe mvivu kukanda )

kata madonge, sukuma paka mafuta zikunje kisha funika 10minutes.
kama una muda zirudie tena kusukuma kupaka mafuta kunja kisha funika tena .

sukuma kaanga katika frying pan iliyokwisha pata moto, make sure na moto sio mdogo sana wala mwingi sana
[ATTACH=full]178330[/ATTACH]

@BAK1 mwalimu wangu :smiley:
uje na maini

Hahahahaha lol! Umenikumbusha ule usemi wako. Kuhusu chapati na mduara. Ila si ulisema siku hizi umekuwa mtaalamu mkubwa hata mduara chapati unauweza.

Umenikumbusha Kenny garden arusha na pale Galaxy,kwa moshi ipo mizuri sana pale mkulima bar ila kwa dar sijawahi kuulizia.

Kwamba chapati kuiva shape waachie mamodel lol

Naam mamodel shurti warembe mduara wa uhakika utadhani kuna mashindano ya miss mduara wa chapati LoL!

Pale sinza kumekucha kwenye kijiwe cha mbuzi