Mahitaji
Changu wazima au vipande
Limao
Chumvi
Pilipili
Mafuta
Jinsi ya kutengeneza
Osha samaki, toa matumbo na uwachanje chale
Twanga pilipili na chumvi kwenye kinu, ukipata paste iweke kwenye bakuli uikamulie limao
Paka paste ya chumvi, limao na pilipili kwenye samakii
Acha amarinate ikiwezekekana weka kwenye chujio la nazi chini weka sufuria ya kukinga maji.
Unaweza kuwaweka kwenye ungo ukaanika darini kama hakuna kunguru, mimi huwa ninaweka kwenye fridge kwa masaa 12.
Kukaanga, acha mafuta yapate moto, usipende kupika na moto mkali, kama ni jiko la umeme namba 4 inafaa
Samaki wa kukaanga kwa ugali, au wali maharage raha sana.