Bongo Movies zinafanya watanzania tuonekane wapumbavu.

Kwa kweli hizi dialogues za kwenye Bongo Movies ni za kijinga kupita kiasi. Leo nip0 safarini wameweka Movie ya Kigosi. Kigosi anajiita shedrack na amempenda binti anaitwa Tresha. Basi Kigosi humo anaongea utumbo Tena kwa kupayuka hatari. kama alitaka ile iwe movie ya Vichekesho amefeli vibaya maana inaudhi badala ya kuchekesha.

Nashauri bongo movie mtafute watu wa kuwaandikia scripts. Siyo mtu aongee kinachokuja kichwani sehemu kubwa mnaharibu. Pia muongee kwa utulivu, hili ni muhimu sana. mkipayuka mnaudhi sana. mbona kuna zile movie kuhusu madawa ya kulevya za Bagamoyo wametulia na hadi raha kuwasikiliza. Mbona movie za majuto za zamani zile za VHS zilikuwa poa. Badilikeni, mnaweza kuteka soko la movie EA&DRC mkiacha ujinga.

Ray Huwa Anapayuka Hata Akiongea Na Mama Yake(Kwenye Movie Lakini):smiley:

Mi nilishaachaga kabisa kuangalia hzo movie

Safarini huwezi ziepuka. Zinafanya safari iwe ngumu. earphones hazifui dafu. Hapa wameweka Nyingine jamaa kapendwa na jini linaitwa Clara linataka kumpeleka bahari ya saba kufunga ndoa. Utafikiri watoto wanacheza kibabababa. Wanatupia na soundtracks za metal!! Kilakitu kipo off.

Ni kweli Bongo Movies bado zinamapungufu mengi…

Cc: @Mahondaw

Siangaliagi bongo movie

Mwambie konda awawekee mechi ya belgium…lukaku yupo uwanjani mida hii

Ukweli mchungu Ray hajui kuigiza anaforce tu.

Huyo konda ana kila sababu ya kutiwa makofi. Nani aangalie Bongo Mavie maisha haya?

bongo movie ndo takataka gani iyo?

Bongo movie ni kama gofu waigizaji wamekimbia na kwenda kwenye majukwaa ya kampeni za kijani

Bora nimtazame Dj Afro amigozzz

Kwakweli.

Hao wenye magari nao wapuuzi yanini kuchosha watu na vitu vya kijinga.

Mi nashauri hawa jamaa wangekuwa wanatuwekea tu picha za wanyama. Hizi picha watu wote huwa wanazifurahia, pia huwa zinaamsha mazungumzo. Mabongo movies ni kudumazana akili. Kama ni mtu wa kusafiri mara kwa mara hizi bongo movies ni nuisance kuliko safari yenyewe.

Pole Mkuu…

wenyewe watakwambia “rudi nyumbani kumenoga”!

Labda wanapewa hela na akina Ray wawafanyie promo kwenye magari yao hahaha! Ila wanaboa watu wanaojitambua aisee.

bongo movie zinapunguza uwezo wa kufikiri