Belgium kukutana na Brazil/Mexico Robo fainali? Akikutana na Brazil, ipi itashinda?

Kwa jinsi nilivyoona Belgium wanavyosakata kabumbu huko kwenye Ardhi ya Nchi ya Putin alikoweka Daktari wetu Mabilioni yakeya pesa almaarufu kama Mabilioni ya Urusi, ni dhahiri kabisa Belgium wanauwezo mkubwa wa kufika mbali na hata fainali au kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia.

Kwa sasa hatua ya mtoano ya 16 bora Belgium atakutana na Japan, na nina imani atashinda na kuelekea robo fainali, Brazil katika hii hatua atakutana na Mexico, Mexico ilionesha makucha yake tangu mwanzo ilipoilaza mabingwa wa tetezi-Germany bao 1 kwa nunge, wakati huo Brazil walilazimisha drawl ya na Uswizi ya kufungana bao 1 kwa 1. Katika mechi zilizofuata, Brazil ilishinda lakini sio kwa kiwango cha kuvutia sana ikizingatiwa wakati ilipokutana na Croatia ilishinda kwenye dakika za nyongeza baada ya kushindwa kufunga bao hata moja kwenye dakika 90.

Belgium imeonesha soka la nguvu lenye ustadi wa hali ya juu na kushinda mechi zake zote 3 kwenye hatua ya makundi.

Endapo Brazil atashinda kwenye hatua ya 16 bora ambapo atacheza na Mexico, Jee wakija kukutana na Belgium kwenye hatua ya Robo fainali ni ipi itagaragazwa…

Wadau wa mpira karibuni tutiririke kabisa juu ya tathmini kuhusu mwenendo wa hii michuano hasa hizi timu nilizozitaja hapa

Kuna huyu mtu anaitwa Lukaku, ni hatari sana…

Nyie nao na utabiri wenu…hii world cup itawasuprise sana…

BRAZIL atashinda lkn kwa msaada wa VAR.

Mpaka sasa mpira hauleweki ingawa Brazil na Belgium ni timu zinazopewa nafasi ya kukutana na endapo zitakutana ni 50 kwa 50 yeyote anaweza akufungwa.

mkuu lini brazil amecheza na croatia toka WC ianze

hata hivyo ubeligiji anacheza mpira wa darasani sana anaweza kutolewa kirahisi tu na brazil

Brazil wanaujua mpira wakikutana Na Belgium natabiri Belgium kufungashwa virago

[ATTACH=full]180496[/ATTACH]

mzee baba muhindi atakukula kiulaini kwa hii beti yako

Sorry mkuu, niliteleza kidogo kwenye vifupi vya Croatia (CRO) na Costa Rica (CRC) ndio nikataja Croatia,
Iilikutana na Costa Rica iliposhinda kwenye dakika za nyongeza

Upande waliopo England ni mwepesi sana kwa mtazamo wangu.

Hata mimi naona hivyo, England waliona bora wafungwe waje upande huo

fainali ni Russia vs Japan

ile bangi bado haijaisha kichwani usiku mwema

Siyo kwa brazil hii

belgium brazil spain mmojawapo anabeba ndoo

Vijapan visumbufu sana. Belgium akiweza kuvivuka atafika mbali

Belgium nimeitabiria kufika fainali ila kwenye kubeba ndio hapaeleweki

Zile hat trick za mechi ya kwanza mbwembwe zoote zimeishia leo kijiti cha magoli kinaendelea kwa Kane na Lukaku

Ndoo anabeba france…

World Cup siyo Kwa Kila nchi.Lipo Kwa ajili ya nchi chache