Battle: Dar Es Salaam vs Nairobi

Wadau waliokuwepo kule jamiiforums ya Dar, sijui kama wote wanataarifa kaam kuna jamiiforum ya Nairobi huku,moja ya thread iliyopata wachangiaji wengi ni Dar vs Nai,
Hatutaki matusi ,tulikua tunapost majengo,miradi mipya ya zamani na mipya kwenye hii miji mikubwa, sehemu za starehe,usafiri,barabara,tallest buildings na mengineyo.
Karibuni

Ngoja @annael @Motochini @ichoboy na wengine waje

Team kibera mpoooo!??

@kadoda_jizee_la_60s

tupo kama kawaz.

binafsi nimevunjika moyo, morali niliyokuwa nayo kule jf katika kuitetea nchi yangu mbele ya wakenya, yote imefutika.

magufuli katurudisha hatua mia moja nyuma.

Kweli kabisa mkuu

Kweli kabisa MTU ulikuwa mbali Data zote kule za kuanzia 2006~2018
Hazipo hewani, biashara za watu na mambo mengine yamefutika

kwasasa sitojisumbua tena kutoleana mapovu na jirani zetu wakenya kuhusu tanzania.

nilisha play part yangu kule jf ya kutetea nchi yangu mbele ya wakenya tangu mwaka 2011 mpaka siku ya mwisho wahusika walipolazimika kuiondoa hewani.

hapa kenyatalk nitakuwa napiga soga tu pale nipatapo nafasi. sitokuwa na mda wa kuzama katika serious debate.

Serikali inavyoongoza ina dissapoint sana watu

Watanzania tulio wengi timevunjika mioyo yetu sana kiasi ya kwamba imekua ngumu sana kusimama kidete kuitetea Tanzania ktk nyanja mbalimbali za uchumi, jamii na siasa. Kitendo cha TCRA kutunga sheria ngumu kwa wamiliki wa miyandao ya kijamii.
Jamiiforums imekua jukwaa langu pendwa sana na pindi walipolazimika kufata amri ya tcra ya kusitisha huduma, nilikerekwa sana.

kadoda karibu kenya talk

Eti mwanakijiji wa shule ya chekechea anamwambia mwanakijiji mkongwe karibu Nyalgunga! :smiley: Vipi @colloh-Mzii na jizee_la_60s? Mpo eeh? I see you ma niggaz. :smiley:

Kumbe nawe nigeni nyumbani kwako

nimetumia account ingine hamngenijua

Ahaa, sawa sawa nimekusoma mkuu. Karibu tuendeleze midahalo yetu kama ilivyoliwa awali ndani ya jf

nimekaribia, ila huku nimekuja tu kujipumzisha… sijaja kufanya battle na wakenya.

Vita ikiisha kule nyumbani, utarudo kuendeleza bato?

Nimekubali, Jiwe kiboko yao. Yaani ghafla watz wote wakawa walokole. Hamna tena zile battle na ligi??? Bwana asifiwe!

sina mda huo tena… nilishatimiza wajibu wangu tangu mwaka 2011 mpaka ile siku jf ilipositisha huduma yake.

after all jf itakayorejea haitokuwa kama jf ile iliyopita,kutakuwa na kiwango kikubwa sana cha censorship.

unafurahi kuishi bila battle na watz?.