Bajeti ya Tanzania imepita kwa mabavu!

Ndivyo ninavyopasa kusema kuwa bajeti ya Tanzania imepita kwa mabavu. Wabunge wamepigwa mkwara na Spika Job Ndugai, kuwa ni lazima waipitishe bajeti hiyo, kinyume chake watakiona cha moto kwa kuwa Rais atalivunja Bunge mara moja na wabunge wengi majina yao hayatarudi majimboni!

Hivi pamoja na kutamka hivyo Spika bado anaamini kuwa Bunge lake ni mhimili unaojitegemea na siyo kuwa linaendeshwa kwa remote control toka Ikulu??

Hivi kwa matamshi ya Spika Ndugai hayajavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005, ibara ya 3(1) ambayo inasema nchi yetu iko huru na ni ya kidemokrasia??

Hivi hii ni serikali gani ambayo siyo sikivu na kuamua kuweka pamba masikioni kwa kilio cha wananchi wake??

Hivi hii serikali haijasikia vilio vya wananchi wake kupitia kwa wabunge wa mikoa ya Kusini wa CCM, akina Nape Nnauye, Hawa Ghasia pamoja na wabunge wa upinzani akina Bwege, Katani na wengine??

Hivi inapofikia Mbunge anadiriki kumwaga chozi bungeni kutokana na wale anaowawakilisha kuibiwa pesa yao ya korosho, bado kweli Spika wa Bunge anadiriki kuwapiga mkwara wabunge hao kuwa ni lazima waipitishe bajeti hiyo ama sivyo watakiona cha moto, hivi kweli hiyo ni kauli ya kiungwana kweli??

Hivi inapotokea Mbunge anajiapiza kuwa Waziri Mpango askanyage tena mikoa ya Kusini ya Mtwara na Lindi, hivi watawala wetu wanaiona kauli hiyo kuwa ni ya kawaida na hawaoni sababu ya ku-reverse sheria yao ya “kijinga” ya ku-centralize mapato yote ya serikali hii kupitia kwake Mpango na mtoto wa dadake Magufuli, Doto James ambaye ndiye anayeyadhibiti mapato yote ya nchi hii??

Hivi Mkulu anapojigamba kuwa kiuchumi “we are on the right track” hivi siyo kwamba walio katika hiko kitu kinachoitwa “right track” ni yeye Magufuli na watu wanaomzunguka akina Bashite??

Ee Mwenyezi Mungu tuepushe na adha hii ya huyu mtu anayeitwa Magufuli ambaye ni dhahiri amedhamiria kuitosa shimoni nchi hii ya Tanzania

Nimesikiliza hii video,huu ndio ukweli wenyewe kutokana na Katiba ya Tanzania kama Magufuli angelivunja Bunge…,Ukweli ni kwamba kama Raisi atavunja Bunge la na yeye Raisi itabidi aachie Kiti cha Uraisi,Bunge likivujwa moja moja nchi inarudi kwenye uchaguzi wa raisi…

https://www.youtube.com/watch?v=cq6XZxkzKV4

Yaani Bunge safari hii limepata Spika kilaza haijawahi tokea…

Yeye kazi yake ni kupokea maelekezo toka Ikulu tuuu…

Hivi ina maana gani kusema kuwa Bunge ni Mhimili unaojitegemea na unaoisimamia serikali, kama mhimili huo unaweza kupigwa mkwara wa kitoto kama huo kuwa mkiikataa
bajeti, Rais atalivunja Bunge na wengi wenu hapo majina yenu hayatarudishwa majimboni??

Hii nchi kweli this time tumepatikana, hivi kweli huyu Mkulu kwa haya mambo anayoyafanya nchini, tuna haki ya ku-doubt kama kweli huyo Mkulu yupo sawa upstairs!

Na kinachompa kiburi ni hayo magari ya Polisi ya washawasha, ambayo yeye kama Commander in Chief atayaamrisha yaje yazime protest yoyote itayotokea hapa nchini!

Hmm!..

Bunge Ni mhimili unaojitegemea

Ile staili ya kupiga kura sio kabisa. Wangeruhusu ipigwe kura ya siri kama ingepita kwa kishindo…!!

Ila umeingiliwa na mhimili uliojichimbia mzizi mrefu sana.

Nashangaa woga wa nini?

Kama kweli wanajiamini kuwa wanawatendea haki ni kwanini wapige kura ya wazi, tena baada ya Spika wa Bunge kupiga mkwara mzito kuwa, wabunge wakiigomea bajeti hiyo,Rais atalivunja Bunge hilo mara moja na uchaguzi ukirudiwa, wengi wa wabunge wa sasa majina yao hayatarudi

Kuungoa yahitaji nguvu ya ziada

Huu msimu tuna spka kilaza kweli kweli

Huyu jamaa alimpiga mgombea mwenzake bakora hadi akazimia na nusura amtoe maisha…

Nawashangaa wabunge wa CCM ndiyo wamemkabidhi “Muuaji” kiti cha Spika!

Sasa unafikiri wangefanyaje na wabunge wenyewe wanajali matumbo yao tu?
Tulikofikia ni Bwana pekee awezaye kutuokoa

CCM janga la taifa…,Mauaji na vitisho ndio njia yao mpya ya kuwaongoza watanzania

Wabunge wa ccm hawajitambui wala kujielewa. Kama kweli uko kwa ajili ya mwananchi unaona shida gani bunge likivunjwa? Maana baada ya hapo hata huyo aliyevunja na yeye anasombwa na maji.

Jiwe lingeachiwa livunje bunge ili tuondokane na hili jinamizi !!