Akina Mwigulu nao wamehamia KenyaTalk?

Jamiiforums ilikuwa na members mbalimbali wakiwepo viongozi wa serikali,wabunge nk(Juliana Shonza,Mwigulu Nchemba) Hawa ni baadhi tu.Na wale team Lumumba akina Jingalao.Hivi Hawa nao wamehamia KenyaTalk?

Hakika watasoma kama guest au kuhamia tu kwa Id’s tofauti…maana ushauri,maoni na ushahidi wa jf uliwasaidia sana kwenye kazi zao za kila siku ingawa walikuwa hawatoi credit kwa jf

Yaani hapa kama wamepigwa Pini wakisema wajiunge huku itakuwa kama kumbe walikuwa wanaipenda jf hivyo wanamsaliti mkulu,wasipojiunga watakuwa wanakereketwa kujibu mambo mbalimbali Nadhani watakuwa kama guest users kama ulivyosema

Hahah!! Umenikumbusha Jingalao

Wanapita tu huku kuperu peruzi kwa wizi

Mimi nakumbuka nilishawahi ku-report taarifa iliyosaidia kukamatwa kwa wauwaji ambayo niliipata mahala mtaani nikairusha JF baada ya siku kadhaa nikapta inbox msg ya kunishukuru kwamba habari ile imewasaidia sana. kwa hiyo kufutwa kwa JF hapa kilichotokea ni loose loose situation. Naamini kabisa JF iliisaidia sana serikali hasa police.
Jamaa waliuwa mtu ndani ya gari barabarani kwenye foleni wakakimbia walikuwa na pikipiki. Mimi nipo kijiwe kimoja nikakuta jamaa wanaongelea jambo lile alielifanya, jina lake hadi jina lake la utani na anakaa wapi.

UNAFIKIRI HAWALIJUI HILO,TATIZO NI MALAIKA WA MITANDAO

Wamajitoa ufahamu tu

Malaika jiwe kafurahi kwelikweli.

Anafurahi nini wakati RAIA wanakomenti kama kawa huku ukimbizini?

Mwigulu yumo, si ndo anaitwa stroke? hahahh just kidding

JF was supportive in every aspect, na mazuri yake yalikuwa mengi kuliko mabaya yake, but now ipo ICU, ikitokea Mungu akaipenda zaidi, itabidi tusubiri parapanda itakapolia, hamna namna ingine ‍♂️‍♂️‍♂️!

apeleke server usa baby

Wanatucheki tu halafu wanasema hiiiiii!
Nalog off

Watahamia kwa ID ambazo hutoweza kubaini kama ni wao…

Cc: @Mahondaw

mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm! kweli serikali ya Tz ilikuwa inakula na kipofu ikasahau ikamkamata mkono. Sasa huku hawawezi kuja kweli?

[FONT=courier new]Kwani aliyekuambia hata huyo ’ aliyewaamuru ’ TCRA kufanya walichotufanyia siyo Member wa JF ni nani Mkuu / Villager?[/FONT]

Tunawakaribisha sana kwani JF iliwarahisishia sana kujenga hoja

Lazima wahamie ni sawa na nyumba za ibada, unakuta wale watu waliopo kwenye mstari wa mbele ktk maswala ya imani, ukifatilia ndio wachawi namba moja