Adam Malima; Hili Suala la Tarime Unajishushia Hadhi

Nimekusikia ukielezea jinsi mfanyabiashara Wa Tarime Peter Zakaria alivyojitetea na kupambana asitekwe na hao maafisa wako Wa usalama ila we we ukielezea kama vile yeye ndio kafanya uhalifu.
Habari za huko Tarime na kutoka kwa mashuhuda akiwamo kiongozi Wa ccm huko ni kuwa kulikuwa na njama za kumteka kama alivyo potea mmiliki Wa mabasi ya Samry bw Simon na kuokotwa kwenye kiroba mtoni.
Jee kwani lazima afisa usalama afanyapo jinai lazima serikali imtetee?
Ulionekana una msimamo Wa kiongozi Wa kisasa lakini hizi kauli ZINAKUSHUSHIA HADHI. Au unalinda dhibe yako?

mungu kawaumbua hawa mashetan wa jiwe

Mkuu kwani huyo Adam Malima ana heshima yotote anayoilinda. Haimaanishi mtu akiwa na madaraka ana heshima. Huyo Malima ni mmoja wa watu wenye siasa za majitaka na anaeleweka. Ukitaka kujua hilo jambo lina mkono mchafu angalia anayetoa taarifa ya tukio ni RC ns sio RPC.

Ulitegemea afanye kinyume mkuu?

Huyu jamaa inaonekana aliombwa fungu akawatolea za mbavu sasa naona wameona wadili nae.

Walitaka kumteka huyu, hii nchi imefika pabaya

Hapo kuna zaidi ya tatizo…hawa wafanyabishara wakubwa huwa wanashirikiana na maafisa usalama kwa mambo mengi ya nyuma ya pazia.

Hapo ukiona hivyo ujue dili lilikaribia kubumbuluka au wamedhurumiana, hivyo wanachofanya ni kukupoteza tu.

Usicheze dili lolote na maafisa usalama, ipo siku watakugeuka tu.

Msukuma alisema Bashe hakutekwa na Usalama,angetekwa na Usalama asingepelekwa Polisi Ila… Maneno mengine nimeyasahau

Ukisikia PAAAA…ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha…amefanya makosa
Ukisikia PAAAA…ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha…amefanya makosa

Mkuu najaribu Ku attach conversation za watu mbali mbali mashuhuda nashindwa huu mtandao sijaujua vizuri.
Ila story iliyopo ni kuwa maafisa hao walienda zaidi ya SAA mbili usiku kwenye kituo chake cha mafuta baada ya kumfatilia msibani ambako hakwenda. Walipofika walimshika mateka mtumishi mmoja na kutaka awaeleze yuko wapi, alipoitwa wawili walikuwa nje ya Gari na wandani mmoja aliagiza mpige risasi. Zakaria nadhani ni sharp zaidi yao hivyo yeye aliwawahi na Wa ndani walipoona wamezingirwa na hawawezi kuacha wenzao wamelala chini wakajitambulisha ni kutoka usalama.
Hivyo hata kupelekwa Polisi ni Zakaria na RAIA waliowapeleka hao watu Polisi na kibao kikageuzwa huko.
Serikali chini ya RC inajivua nguo kabisa. Yaweza kuwa kweli Zakaria na dili zake chafu, lakini Govt haiwezi nayo kufanya mambo yake kinyume cha sheria kama nao ni wafanya dili

hiz habar zinachanganya, ngoja niendelee kudadavua.

Mkoa wa Mara haujawahi kumpandisha mtu hadhi, hasa hawa wanasiasa.

Subiri na yeye hadhi yake ishuke arudi alikotoka.

[FONT=tahoma]Hatari kubwa walitaka na yeye wampoteze watu wasiojulikana akawa amewawahi kama alikuwa anahitajika na vyombo vya dola kwann asingetumiwa wito mara moja kuliko kujaribu kumteka/kumchukua kwa nguvu[/FONT] ikabidi na yeye ajihami maana sidhani kama walionyesha vitambulisho vyao.

Maelezo ya rc yanazua maswali mengi; sijui kwanini hakumwachia tu RPC aeleze hiyo narrative. Hata ingekuwa kumchukua Zacharia kwa mahojiano wa kufanya hiyo kazi ni Polisi na siyo Tiss.

Angepelekwa wapi sasa? Mtoni kwenye viroba?

Hivi huyu Malima amesahau alivyodhalilishwa na vyombo vya usalama pale Dar!

Kutesa kwa zamu yake itapita

Duh inaonekana kuna mengi zaidi.!

Wanajidharirisha sana aisee

Sijui kwanini Zacharia hakuwamaliza kabisa…
Maana picha ninayoipata ni kwamba wangeondoka nae sidhani kama angekuwa hai mpaka hivi sasa.

Mkuu habari ndio hiyo. Halafu kitendo cha kumuona RC tu anatolea maelezo hilo tukio la uhalifu nikajua waongozaji wa watu wasiojulikana wameanza kujitokeza. Nimeona kule twitter John Heche akitolea mashaka RC kuongelea hilo jambo, kuna jamaa naona ni huohuo usalama wa wasiojulikana wakamtishia ile mbaya. Ni kikundi kikubwa kiko mitandaoni kwa kazi maalum.