Adam Malima; Hili Suala la Tarime Unajishushia Hadhi

Mshangai

Senior Villager
#1
Nimekusikia ukielezea jinsi mfanyabiashara Wa Tarime Peter Zakaria alivyojitetea na kupambana asitekwe na hao maafisa wako Wa usalama ila we we ukielezea kama vile yeye ndio kafanya uhalifu.
Habari za huko Tarime na kutoka kwa mashuhuda akiwamo kiongozi Wa ccm huko ni kuwa kulikuwa na njama za kumteka kama alivyo potea mmiliki Wa mabasi ya Samry bw Simon na kuokotwa kwenye kiroba mtoni.
Jee kwani lazima afisa usalama afanyapo jinai lazima serikali imtetee?
Ulionekana una msimamo Wa kiongozi Wa kisasa lakini hizi kauli ZINAKUSHUSHIA HADHI. Au unalinda dhibe yako?
 
idawa1

Senior Villager
#6
Hapo kuna zaidi ya tatizo...hawa wafanyabishara wakubwa huwa wanashirikiana na maafisa usalama kwa mambo mengi ya nyuma ya pazia.

Hapo ukiona hivyo ujue dili lilikaribia kubumbuluka au wamedhurumiana, hivyo wanachofanya ni kukupoteza tu.

Usicheze dili lolote na maafisa usalama, ipo siku watakugeuka tu.
 
Mshangai

Senior Villager
#9

Mkuu najaribu Ku attach conversation za watu mbali mbali mashuhuda nashindwa huu mtandao sijaujua vizuri.
Ila story iliyopo ni kuwa maafisa hao walienda zaidi ya SAA mbili usiku kwenye kituo chake cha mafuta baada ya kumfatilia msibani ambako hakwenda. Walipofika walimshika mateka mtumishi mmoja na kutaka awaeleze yuko wapi, alipoitwa wawili walikuwa nje ya Gari na wandani mmoja aliagiza mpige risasi. Zakaria nadhani ni sharp zaidi yao hivyo yeye aliwawahi na Wa ndani walipoona wamezingirwa na hawawezi kuacha wenzao wamelala chini wakajitambulisha ni kutoka usalama.
Hivyo hata kupelekwa Polisi ni Zakaria na RAIA waliowapeleka hao watu Polisi na kibao kikageuzwa huko.
Serikali chini ya RC inajivua nguo kabisa. Yaweza kuwa kweli Zakaria na dili zake chafu, lakini Govt haiwezi nayo kufanya mambo yake kinyume cha sheria kama nao ni wafanya dili
 
Kijereshi

Senior Villager
#12
Hatari kubwa walitaka na yeye wampoteze watu wasiojulikana akawa amewawahi kama alikuwa anahitajika na vyombo vya dola kwann asingetumiwa wito mara moja kuliko kujaribu kumteka/kumchukua kwa nguvu ikabidi na yeye ajihami maana sidhani kama walionyesha vitambulisho vyao.
 
idawa1

Senior Villager
#17
Mkuu najaribu Ku attach conversation za watu mbali mbali mashuhuda nashindwa huu mtandao sijaujua vizuri.
Ila story iliyopo ni kuwa maafisa hao walienda zaidi ya SAA mbili usiku kwenye kituo chake cha mafuta baada ya kumfatilia msibani ambako hakwenda. Walipofika walimshika mateka mtumishi mmoja na kutaka awaeleze yuko wapi, alipoitwa wawili walikuwa nje ya Gari na wandani mmoja aliagiza mpige risasi. Zakaria nadhani ni sharp zaidi yao hivyo yeye aliwawahi na Wa ndani walipoona wamezingirwa na hawawezi kuacha wenzao wamelala chini wakajitambulisha ni kutoka usalama.
Hivyo hata kupelekwa Polisi ni Zakaria na RAIA waliowapeleka hao watu Polisi na kibao kikageuzwa huko.
Serikali chini ya RC inajivua nguo kabisa. Yaweza kuwa kweli Zakaria na dili zake chafu, lakini Govt haiwezi nayo kufanya mambo yake kinyume cha sheria kama nao ni wafanya dili
Duh inaonekana kuna mengi zaidi.!
 
#19
Sijui kwanini Zacharia hakuwamaliza kabisa..
Maana picha ninayoipata ni kwamba wangeondoka nae sidhani kama angekuwa hai mpaka hivi sasa.
 
Last edited:

Tindo

Village Elder
#20
Sijui kwanini Zacharia hakuwamaliza kabisa..
Maana picha ninayoipata ni kwamba wangeondoka nae sidhani kama angekuwa hai mpaka hivi sasa.
Mkuu habari ndio hiyo. Halafu kitendo cha kumuona RC tu anatolea maelezo hilo tukio la uhalifu nikajua waongozaji wa watu wasiojulikana wameanza kujitokeza. Nimeona kule twitter John Heche akitolea mashaka RC kuongelea hilo jambo, kuna jamaa naona ni huohuo usalama wa wasiojulikana wakamtishia ile mbaya. Ni kikundi kikubwa kiko mitandaoni kwa kazi maalum.
 
Top